Jeshi la Polis mkoani Kagera linawashikilia watoto watatu,kwa tuhuma za kumpiga fimbo baba yao mzazi na kumsababishia kifo.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polis mkoani Kagera Gilles Muroto,alisema tukio
hilo lilitokea mnamo mwezi Septemba 15,katika kijiji cha Mkunyu kata
Kikukuru tarafa Mabira wilayani Kyerwa,ambapo watuhumiwa hao ambao
hawakutajwa majina yao kutokana na umri wao kuwa chini ya miaka
18,walimuua baba yao mzazi Henry Siliakus(62)kwa kumchapa fimbo hadi
akapoteza uhai wake.
Muroto alisema watoto hao ambao kati yao mmoja mwenye umri wa miaka 17
anasoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Mkunyu,huku mwenye
umri wa miaka 13 ni mwanafunzi wa darasa la nne na mwenye umri wa miaka
11 ni mwanafunzi wa darasa la tatu, wote wakiwa wanasoma katika shule za
msingi Mkunyu.
Alisema mzazi huyo alikumbwa na mauti hayo kutokana na kupigwa fimbo
nyingi kichwani akiwa nyumbani kwake,huku sababu ya awali ya mtafaruku
huo uliosababisha kifo ikidaiwa kuwa ni ugomvi wa baba na watoto
wake,kwa kile kilichodaiwa marehemu kuwa na tabia ya kuuza chakula cha
familia na kuwaacha watoto wakitaabika.
Hata hivyo,alisema jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu
ya tukio hilo na litawafikisha mahakamani watoto pale taratibu za
kisheria juu ya umri wao zitakapokamilika. ITV
No comments:
Post a Comment