Hayo
yameonekana Leo Jijini Dar es Salaam wakati waandishi wa Habari
walipokuwa wakichukua taarifa za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alipokuwa polisi Makao makuu,
Ambapo
Polisi walikuwa wakilinda ulinzi maeneo hayo walikuwa wakiwazuia
waandishi na kuwafanyia unyama wa hali ya Juu ikiwemo kuwapiga hadi
kuwapelekea maumivu katika sehemu mbalimbali za mwili.
Akizungumza
na Mwandishi wa Mtandao huu juu ya Unyama aliofanyiwa na jeshi la
Polisi Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Tanzania Daima Josephati
Issango alisema anasikitika sana kwa Jeshi la polisi kumfanyia unyama
huo huku wakijua yeye ni mwandishi
“hivi
Jeshi la Polisi tumelikosea nini maana mimi hapa na peni na kitabu tu
nachukua taarifa sasa leo wananifuata na kunipiga tena wanivunja
mguu,na kunipora vifaa vyangu nilivyonavyo kwa kosa lipi wakati kazi
yangu mimi ni kuchukua taarifa tu”alisema Issango
No comments:
Post a Comment