Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma
Nkamia akitoa hutuba
yake kwenye uzinduzi wa Nembo ya radio Triple A fm na kuwataka wamiliki
na wanahabari kuhakikisha wanafuata maadili ya taaluma ya uandishi wa
habari iwe kazini au nje ya
kazi zao.
Serikali
imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo kiuka
maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo
hivyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari vijana utamaduni na michezo
Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku
akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia
jamii
bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa
amani.
Naibu Waziri wa habari vijana utamaduni na
michezo Juma Nkamia akiwa na
Bodi ta wakurugenzi wa Kampuni ya The Blue Triple A Ltd ambayo ni
kampuni tanzu ya Radio Triple A fM inayoongozwa na Mkurugenzi wake kulia
na kushoto Mr&Mrs Papa King Mollel wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya naibu waziri kuzindua nembo ya Radio hiyo jijini
hapa
Nkamia alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
"Lengo
hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio kichocheo cha
uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima la
kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na
jamii"alisisitiza Nkamia
Kwa
Upande wake Meneja wa Tcra kanda ya kaskazini Anethy Matindi aliwakemea
mablogger kwa kupachika picha zinazo vunja sheria za nchi ikiwemo pia
kupachika picha
zisizofaa kwa jamii na kuwa dawa yao ipo inakuja
Baadhi ya viongozi wa serekali wa jiji la Arusha
nao waliudhuria uzinduzi huo.Matindi
alisema kuwa imekuwa ni tabia kwa vyombo vya habari kutofuata maadili
hivyo akavitaka kuacha mara moja kutumia vyombo hivyo kwa kukiuka
taaluma na weledi wa tasnia hiyo
Naye
meya wa jiji la Arusha Gaudency Lyimo alisema kuwa anaipongeza Triple A
Fm kwa kuweza kusogeza habari kwa jamii ya wakazi wa jiji la Arusha
ambapo taarifa zimekuwa zikifika kwa wakti hivyo kuchangia kukua kwa
sekta mbali mbali na kuleta maendeleo kwa jamii
Meya
wa Jiji la Arusha Gaudensi Lyimo akitoa nasaha chache kwa wageni
waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa blue Frem uliopo kwenye
klabu ya usiku ya TRIPLE A NIGHTY CLUB ya jijini
hapa
Mkurugenzi
wa The Blue Triple A Ltd Papaa King aliwashukuru viongozi wote
waliohudhuria katika uzinduzi huo huku akitabaisha kuwa Redio hiyo
itafuata taratibu zote za kisheria katika kujiendesha ikiwemo kuwapa
maslahi mazuri wafanyakazi wake iendane na viwango
.
Sehemu ya wafanyakazi wa Radio Triple A fm
wakiwa katika picha ya pamoja
kulia na kushoto kwa naibu waziri Nkamia ni Meneja wa redio hiyo
Fredy Mumburi kushoto ni mkurugenzi
wa redio hiyo Papa king molel baada ya uzinduzi wa
logo ya redio hiyo jijini hapa.
Chanzo: libeneke la kaskazini blog
No comments:
Post a Comment