TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Imekifungia kwa mda,Chuo
kikuu cha tiba na Sayansi IMTU kutofanya udahili kwa Wanafunzi wapya wa
Mwaka wa Masomo 2014-2015,kutokana na chuo hicho kukiuka sheria
inayosimamia Vyuo Vikuu nchini.
Uamuzi huo wa kikifungia Chuo hicho Umetangazwa mda huu
Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini
(TCU) Profesa Magishi N Mgasa wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari
ambapo alisema maamuzi hayo yamefikiwa baada kikao cha Dharura
kilichoitishwa na (TCU) wiki iliyopita na kujadili taarifa ya timu
iliyotathimini chuo hicho,
Ambapo kikao hicho kikabaini mapungufu makubwa katika chuo cha
IMTU yakiwemo matatizo ya uongozi,kukosa wahadhiri wakutosha na wenye
sifa,kutokuwepo na Vifaa pamoja na kudahili wanafunzi bila hata kuwa na
taratibu zilizowekwa na tume,
Profesa Mgasa alisema kwa kufanya hivyo chuo cha IMTU imekiuka
sheria ya namba 5(1),sura ya 346 ya sheria za Tanzania ambayo inakitaka
chuo Kikuu chochote kufuata taratibu zilizowekwa na tume,
Vilevile Profesa Mgasa alizidi kusema baada ya Tume kubaini
makosa hayo,ndipo wamefikia maamuzi ya kukifungia chuo cha IMTU kufanya
udahili kwa wanafunzi wapya wa Mwaka 2014-2015,mpaka pale
itakakaporekebisha mapungufu yaliyotajwa na Tcu,
Pia tume imetoa notisi ya miezi 3 kwa chuo cha IMTU,kuanzia
tarehe 16 mwezi huu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na endapo chuo
hicho kikikaidi basi TCU haitosita kuwachukulia hatua kali ikewemo hata
kukifungia kabisa.
Aidha Profesa Mgasa aliwataka wanafunzi nchini wasijiunge na
chuo Kikuu chochote bila ya kufuata maelekezo kutoka Tume ya vyuo Vikuu
nchini (TCU).
No comments:
Post a Comment