27 September, 2014

DIAMOND " KUSEMA UKWELI SINA MAHUSIANO NA MENINAH. KILA MTU ANAJUA MIE WANGU NI WEMA"

Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah,  Diamond alisema kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.

“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema superstar huyo wa muziki wa Bongofleva Tanzania.

 “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua kabisa siwezi kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua utaongea na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa kimya,” ameongeza Diamond anayetusua shows katika nchi mbalimbali ndani na nje ya Africa kwa sasa.

“Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi mie nataka kumuoa Meninah’. Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah. Kila mtu anajua mie nina mahusiano na Wema.

“Wema ndo mpenzi wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu hawawezi kumchukia!

Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti” alisema Diamond.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...