Chanzo cha habari hii kilicho karibu na wawili hao kilipigilia msumari wa uwepo wa penzi motomoto kati ya wawili hao kwa kudai hata ukaribu wa msanii Jux na Vanessa ulioripotiwa hivi karibuni katika vyombo vya habari, ulikuwa ni upambe tu kwa Dimpoz.
“Jux alikuwa mpambe tu kwa Dimpoz wala hakuwa na uhusiano na Vanessa kama wengi walivyokuwa wakifikiri,” kilisema chanzo hicho.
“Hatujawahi kugombana hata siku moja na sina jinsi ya kuepuka kufanya naye chochote maana kama ishu ya mapenzi kati yetu ipo wazi na hakuna jipya ambalo naweza kusema watu wakanielewa,” alisema Ommy Dimpoz.Alipoulizwa Vanessa kuhusiana na uhusiano wao, aliishia kucheka tu na kudai hakuwa na cha kuzungumza.
No comments:
Post a Comment