19 September, 2014

DIVA: "ZITTO NI MUME WANGU"


Loveness Malinzi (Diva) mtangazaji wa radio ame charuka na kihoja kipya  baada ya kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV kuruka kilichomhusisha Zitto Kabwe ambapo alipoulizwa kama ameoa au anatarajia kuoa alijibu bado yupo yupo kwanza na kwamba hana mchumba wala mke! Diva ana dai yeye ni mke anayetambulika kisheria  na amesema hayuko tayari kuachana naye kirahisi kwasababu aliishi nae kama mke na mume nyumbani kwa Zitto huko Osterbay jijini Dar kwa zaidi ya miezi sita (6)!
Diva siku za hivi karibuni aliripotiwa kutoka na msanii Crayz GK, lakini  kabla  ya GK, vyombo vya habari vilishawahi kumripoti Diva kutoka na msanii wa Kenya Prezzo!! Sasa hapa ana tuchanganya huyu dada, mara Zitto ni mume wake, mara GK, mara Prezzo....


Hata hivyo gazeti pendwa la Global Publishers lilipotoa habari hii ya madai ya Diva kwa Zitto kuwa ni mume wake,  inasemekana Zitto alikuwa disappointed sana kwasababu madai hayo yanamharibia sana Zitto kisiasa na kwamba maadui wa Zitto watatumia mwanya huo kumharibia!!  Turudi nyuma, kuna habari iliyowahi kuripotiwa katika gazeti na blogu , kichwa cha habari kikiwa Diva wa Clouds amtega Mhe. Zitto, twende pamoja kusoma hapo chini


MTEMEA maiki wa Kituo cha Redio cha Clouds FM cha jijini Dar es Salaam, Loveness Malinzi ‘Diva’, mapema wiki hii alifanya mahojiano ya kimapenzi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Zuber Kabwe (pichani) huku maswali yake yakiwa ya mitego zaidi, kitendo kilichomfanya mheshimiwa huyo kutumia uzoefu wake kujibu.

Mahojiano hayo yaliyojaa ung’eng’e mwanzo mwisho, yalisikika siku ya Jumanne usiku kupitia kipindi kilichojinyakulia mashabiki wengi cha Ala za Roho chini ya mtangazaji huyo.
Swali la kwanza aliloulizwa Kabwe ni kama ana mpenzi au la ambapo alikiri kuwa na mchumba ambaye hakumtaja jina.

Baadaye aliulizwa kama anaamini Siku ya Wapendanao Duniani, lakini mbunge huyo machachari alisema haamini siku hiyo kwa sababu kila siku yeye na mpenzi wake ni Valentine.

Hata hivyo, Diva alivuka mipaka pale alipomuuliza mbunge huyo swali ambalo hakulielewa hata pale alipofafanuliwa vizuri, alishindwa kulijibu kwa wakati.

Ifuatayo ni sehemu fupi ya mahojiano hayo;
Diva: ‘Do you kiss and tell?’
Kabwe: Mh... ‘I don’t get your point’.

Diva: Yaani una kanuni za kutoa siri zako za mapenzi nje kwa rafiki zako? Mfano labda umetoka na msichana fulani kisha unawaambia jamaa zako?
Kabwe: Hapana, sina kanuni hiyo, ‘I can’t...

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...