Lady
Jay Dee wako kwenye wakati mgumu wa ndoa yao.Akizungumza
katika Exclusive Friday ya 100.5 Times Fm, Gardner ameeleza kuwa hizo
ni taarifa zisizo za kweli ambazo amekuwa akizisikia tu.“Hakuna
tatizo. Kusema ukweli nimekaa na Lady Jay Dee kwa miaka mingi sana na
hii sio mara ya kwanza kuzungumzwa kwa mambo kama hayo. Na tumeshazoea.
Hata kama kuna kitu kinazungumzwa, mimi hata sina habari kwa sababu
nimeshazoea. Kwa hiyo na mimi pia nimesikia kama ulivyosikia wewe.
Lakini tatizo hakuna.” Amesema Gadner.Ameeleza
kuwa chanzo cha tetesi hizo kinaweza kuwa siku ambayo yeye alionekana
polisi katika kesi ya usalama barabarani na Lady Jay Dee hakufika.
Amesema huenda watu walichukulia tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemshauri asiende ili kuepusha attention zaidi.
“Na
kwa watu kuzungumza…unajua Jay Dee ni mtu mashuhuri, ni mkubwa sana.
Kiasi kwamba kitu kidogo tu kikitokea, hata akijikwaa kinazungumzwa kwa
ukubwa huo. Kwa mfano mimi nimepata shida kidogo ya kesi ya traffic, kwa
hiyo nikamshauri mwenzangu asije pale polisi kwa sababu ya kuogopa tu
vitu kama mapicha na nini. Kumbe watu walinotice kwamba hakuja. Kuanzia
hapo ndio ikaanza ‘aah kuna tatizo..kuna tatizo’.
“Lakini
kwa kweli kuzungumzwa kwa msanii mkubwa kama yule ni jambo la kawaida.
Na ni jambo ambalo ameshalizoea na mimi nimeshalizoea pia.”
Hivi
karibuni Jide alipost picha ya mkono inayoonesha pete yake ya ndoa
kumaanisha uimara wa ndoa yao tofauti na kilichokuwa kikisemwa.
No comments:
Post a Comment