Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya
Bw. Moses Ombati amenukuliwa akisema kuwa mabomu hayo yamelipuka kwenye
mabasi ya abiria mawili tofauti, ambapo Naibu Mkuu wa kitengo cha
kutengua Mabomu, Bw, Eliud Lagat amesema milipuko hiyo imetokana na
mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.
Milipuko hiyo na maafa hayo yamekuja siku moja baada ya watu wanne kuuwawa kwa mlipuko wa bomu ya kutupwa kwa mkono katika kituo cha mabasi mjini Mombasa. Mlipuko mwingine katika ufukwe wa bahari haukuleta madhara.
Kenya imekumbwa na wimbi la mashambulio ya bunduki na milipuko ya mabomu toka nchi hiyo ilipopeleka majeshi yake kupambana na wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al-Shabab mwaka 2011, ambao wameapa kuendeleza mashambulio ya kigaidi kama kulipiza kisasi kwa kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia.

No comments:
Post a Comment