.jpg)
Wolper alisema, katika maisha siku zote anaamini kuna kipindi kinapita
cha kufanya ujana ambacho tayari ameshakipitia na sasa ni muda wa yeye
kutengeneza familia.
“Naamini kabisa huu sasa ni muda muafaka kwangu, niko tayari kabisa kuwa
mke maana nimepitia vitu vingi ambavyo mara nyingi wengi wao huwa
wanakimbilia kwenye ndoa wakiwa bado hawajavimaliza halafu mwisho wa
siku wanazishindwa, mimi nishamaliza vyote,” alisema Wolper pasipo
kufafanua kama tayari ameshampata mchumba au la.
Wolper amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mastaa kadhaa
akiwemo Diamond, Mohamed Mtoro ‘Dalas’ ambaye alimbadilisha dini ili waweze
kufunga ndoa lakini ikaota mbawa.
No comments:
Post a Comment