Kansa Mbaruku - Mgombea Uenyekiti CHADEMA TAIFA
VIONGOZI NA WATUMISHI mashuhuri kadhaa ndani ya ofisi ya MAKAO MAKUU YA CHADEMA, wameonyesha kufurahishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Tabora kupambana na MBOWE kwenye kugombea uenykiti wa Taifa wa CHADEMA.
Wakizungumza na chanzo cha habari hii wakiomba kutokutajwa majina yao humu wamesema kwa sasa watapata pa kupumulia ikiwa MBARUKU ATASHINDA.
''Unajua Mbowe anatufanya sisi kama watoto wake, amekigeuza hiki chama kama chumba chake cha kujisaidia haja kubwa na ndogo, anakifanya anavyotaka, ona alivyojifedhehesha, amemtuma BENSON KIGAILA, akampa Milioni 16 kwenda kigoma kushawishi wazee, badala yake KIGAILA amerudi na wacheza ngoma wa mapigo saba wale. Nimefurahi sana MBARUKU KUTANGAZA NIA. Tutamsaidia chini chini auangushe huu mbuyu uliooza''. Alisema
Naye Afisa mwandamizi MAKAO MAKUU ya CHADEMA kwa sharti lile lile la kutokutajwa jina kwa sasa amesema '' Unajua mbowe alitamani kulia aliposikia MBARUKU amechukua fomu, alipiga simu kila sehemu kutukana matusi mazito mazito, eti tumemruhusu vipi kurudisha fomu? Huyu mwenyekiti sasa anaanza kuchuja vibaya.........nakwambia asipojiangalia sawasawa, lazima aangushwe. Watu mikoani wanamchukia mno, kwa kweli amekuwa DIKTETA zaidi ya IDDI AMINI. Chama hakiwezi kuendeshwa kwa anavyotaka yeye''.
MBOWE alipopigiwa simu ili kuthibitisha minong'ono hiyo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment