OKTOBA
12 mwaka huu katika kuadhimisha siku ya amani duniani viongozi wa dini
wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakiwa
na lengo la kudumisha amani iliyopo nchini.
Mtanange
huo utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wachungaji na Mapadre na
mgeni rasmi katika mchezo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
ambaye tayari amekubali kuungana na viongozi hao wa dini.
Akizungumza
jana jijini, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya mchezo huo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said
Sadick atakuwa mwamuzi msaidizi akisaidiwa na Kamishna wa Kanda Maalumu,
Seleman Kova na Afande IGP Ernest Mangu atakuwa mpuliza kipyenga wa
kati.
Alifafanua
kuwa viongozi hao wa dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya
kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya vizuri katika mtangane huo wa
kuhamasisha amani na ulivu nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa wanaendelea na mazoezi hayo chini ya kocha mjerumani na Serikali
ya Mkoa wa Dar es Salaam, itazipeleka timu mbili mkoani Morogoro kwa
ajili ya kujifua zaidi na mtanage huo utakaokuwa wa kukata na shoka
kutokana na jinsi timu za viongozi hao wa dini zilivyojipanga kucheza
mchezo huo wa amani.
Ili
kujindaa vema na mchezo huo Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la
KAS,Tanzania, Stefan Reith, jana alikabidhi Sheikh kwa Dar es Salaam,
Alhad Salum vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jeszi na viatu.
No comments:
Post a Comment