27 September, 2014

MCHUNGAJI AWASHANGAZA WAUMINI WAKE BAADA YA KUMUACHA MKEWE NA KUOA "DOGODOGO"


MCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu .

Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.
 
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.

Chanzo ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo aliwaambia waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya mwanzo aliifunga akiwa  Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja jina).
 
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi,  watu weweeeeeeeee......,” kilisema chanzo.

Habari zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini, Jumapili moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa wanaume kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na wamekaa nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu, mkorofi na mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape wake wema!!!

Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, chanzo cha habari hii kilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.

Baadhi ya waumini walioweza kuzungumza na chanzo cha habari hii walionesha kushtushwa na kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa tayari kusema neno! 

Baadaye  mchungaji alitafutwa kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
 
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.” 

Baadaye alimtumia ujumbe  mwandishi akiwa ameuandika hivi:
 

“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.” 

Pia chanzo cha habari kilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi huyo kufunga ndoa nyingine.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...