Zaidi ya watu 39 wanasadikiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 79 kujeruhiwa vibaya baada ya mabasi mawili kugongana na kupinduka katika eneo la Sabasaba nje kidogo ya mji wa Musoma, mkoani Mara.
Mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 5 asabuhi, baada ya basi la Mwanza Coach lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na basi la J4 lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Sirari.
Wamesema mabasi hayo ambayo yote yalikuwa kwenye mwendo kasi yalikutana kwenye daraja dogo katika eneo hilo huku pia gari dogo aina ya Land Crusser likitaka kuovateki na hivyo kupelekea kutokea kwa ajali hiyo. Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Nyamhanga amesema alisikia kishindo kikubwa muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo na baadae kusikia vilio vikitokea ndani ya mabasi hayo.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Waandishi wa Habari mkoani Mara Frolence Focus wa Mwananchi na Pendo Mwakembe wa Raia Tanzania wamenusulika kwenye ajali hiyo wakiwa kwenye basi la Mwanza Coach kutokea Musoma.
Akizungumzia kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba 4 hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mra, Frolence amesema walishangaa kuona abiria waliokuwa wamekaa mbele wakisimama na kurudi nyuma na ghafla akasikia mlio mkubwa.
Akizungumza na Redio kahama fm nje ya chumba cha (ICU) kwa niaba ya Mganga Mkuu, Dakatari Martini Khani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa wamepokea idadi kubwa ya maiti na majeruhi huku idadi kamili ikiwa bado haijafahamika.
No comments:
Post a Comment