Allah katika sura Al-Nisa 4:82 anasema kwamba:
Then do they not reflect upon the Quran? If it
had been from [any] other than Allah, they would have found within it much contradiction.
Yaani:
Je, hawaitafakari Quran? Kama isingekuwa
imetoka kwa Allah, hakika wangekuta ndani yake sehemu nyingi zinazopingana.
Ni wazi kuwa kile ambacho aya hii inakisema ni
kuwa, quran haijikanganyi wala kujipinga hata kidogo. Na kutokana na aya hii,
bila shaka Allah pia anamaanisha kuwa kutokuwapo kwa mkanganyiko wowote ndani
ya quran ni kipimo tosha kuonyesha kuwa quran imetoka kwa Mungu wa kweli.
Na hiki kusema kweli ni kipimo kizuri cha kuonyesha
iwapo jambo limetoka kwa Mungu wa kweli au la; maana Mungu wa kweli, kwa kuwa
ni mkamilifu kwa asilimia mia moja, hawezi kusema hivi hapa, kisha aseme
vingine kule – maana yeye hasahau kama mwanadamu. Hawezi kusema, “Nilikuwa na
mambo mengi au mawazo mengi ndio maana nikasahau.”
Kwa hiyo, kimantiki, vilevile kutokana na aya
hii, Allah au Mohammad anamaanisha kuwa, kama tukikuta kuna kupingana ndani ya
quran, basi quran itakuwa haijatoka kwa Mungu wa kweli.
Sasa, kama hivyo ndivyo, hebu tuangalie maeneo
saba yafuatayo (japokuwa yapo zaidi ya haya) ili tuweze kujua, kutokana na kipimo
cha quran yenyewe, kama quran imetoka kwa Mungu wa kweli au la.
Niseme mapema kwamba, mimi si mjuzi wa quran.
Kwa hiyo, ninaweza kuwa niko nje kabisa ya maana iliyokusudiwa. Lakini, nikiwa
kama mtu ninayejaribu kumtafuta Mungu wa kweli, najaribu kujiuliza maswali
katika huko kutafuta kwangu. Hivyo, kama wewe unajua majibu sahihi, nitashukuru
kupata msaada wa maelezo yaliyo sahihi.
Nimetumia maandiko kutoka Kiingereza kwa kuwa
mimi sifahamu Kiarabu; kisha nikayatafsiri kwa Kiswahili:
1.
Sura Al-Baqara 2:109
Many of the People of the Book wish, through
envy, to lead you back to unbelief, now that you have embraced the faith and
the truth has been made plain to them. Forgive them and bear with them until
Allah makes known His will. He has power over all things.
Hapa quran inaongelea watu wa kitabu (yaani
Wakristo), na kusema:
Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao,
wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na
kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia
hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu.
Quran pia inawaagiza Waislamu katika sura Al Imran
3:20 kwamba:
... if they give no heed, then your only duty
is to warn them.
Yaani:
... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi
yenu pekee ni kuwaonya tu.
Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara
2:109 na Al Imran 3:20, tunaona mambo
yafuatayo:
1.Ni wajibu wa Waislamu kuhubiri dini yao lakini
si wajibu wao kuwalazimisha watu kuamini dini yao.
2.Allah kwa wakati wake atawafunulia wale
wasioamini ukweli wa mambo.
3.Ni wajibu wa Waislamu kutoa maonyo tu kwa wale
wanaowahubiria.
LAKINI, HEBU TAZAMA AYA ZIFUATAZO:
Al-Nisa 4:101
The unbelievers are your sworn enemies.
Yaani,
Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa.
Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3
Proclaim a woeful punishment to the
unbelievers.
Yaani:
Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa
wasioamini.
Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39
Make war on them until persecution is no more
and Allah’s religion reigns supreme.
Yaani:
Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso
tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.
Maswali:
1.
Je, aliyempa Muhammad maneno ya 2:109, 3:20 na yale ya
4:101, 9:3, 8:39 ni huyo huyo au ni wawili tofauti?
2.
Iweje aseme kuwa usiwalazimishe watu kuamini bali
waonyeni na kuwavumilia tu, kisha anageuka sehemu nyingine na kusema
walazimisheni, tena kwa vita?
3. Je, hii si ishara ya tabia ya usahaulifu ambayo si tabia ya
Mungu bali ni ya mwanadamu?
4. Kama ni huyo huyo, je, aya hizi zinafanana au
zinapingana?
5.
Kama zinafanana, ni kwa vipi?
6.
Kama zinapingana, huu si ushahidi tayari kuwa quran
haitoki kwa Mungu wa kweli kama ambavyo quran yenyewe imeweka kigezo cha kujua
hilo? Maana Mungu wa kweli hawezi hata kidogo kusahau jambo alilolisema kabla
halafu aje aseme kitu tofauti. Ni viumbe tu ndio wanaweza kusahau na kukosea.
2.
Sura Al-Ankabut 29:6
Quran inasema:
Allah does not need his creatures’ help.
Yaani,
Allah hahitaji kusaidiwa na viumbe wake. (bila
shaka ni katika kutekeleza makusudi na mipango yake).
LAKINI QURAN HIYO HIYO INAWAAMBIA WAISLAMU:
Sura Muhammad 47:7
If you help Allah, He will help you and make
you strong.
Yaani,
Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia
na kuwafanya kuwa imara.
Maswali:
1.
Umesema huhitaji msaada, kisha unasema tena unahitaji msaada! Je, Mungu
anaweza kufanya jambo kama hilo?
2.
Aya hizi zinafanana au zinapingana?
3. Je, hii si ishara kuwa aya hizi zilisemwa tu ili kukidhi mahitaji ya wakati
fulani, lakini msemaji alipoona anahitaji kuwafanya watu watende kinyume chake,
akajikuta amesema tofauti na alivyosema siku za nyuma?
Na tena quran inasema katika sura Al-Baqara
2:244
Fight for the cause of Allah and bear in mind
that He hears all and knows all.
Yaani:
Fanyeni vita kwa ajili ya Allah na mkumbuke
kwamba anaona yote na anajua yote.
Maswali:
1.
Kama kweli Allah hahitaji msaada wa viumbe wake; na kama kweli aliumba
ulimwengu wote kwa NENO TU, iweje NENO hilo hilo lisiweze kuwabadilisha
wanadamu hadi alazimike kuliingiza ndani yao kwa nguvu, kwa vitisho na kwa ukali namna
hiyo?
(Ukristo
unashinda na
kufanikiwa kwa NENO tu. Maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wetu.
Yeye
aliumba kwa Neno; na sisi watoto wake, tunaumba kwa Neno hilo hilo.
Tunahubiri
tu na watu wanaokolewa, wanaponywa, wanalindwa na kusimama na Mungu wa
kweli. Huoni kwamba hii hasa
ndiyo maana ya nguvu ya Mungu? Hatuhitaji kuchinja au kupiga watu ili
wampende
Mungu!! Unawezaje, hata tu wewe mwenyewe, kumfanya mwanao au mkeo
akupende kwa njia ya vipigo na
kulazimisha? yaani, ukitaka mwanao au mkeo akupende utamshikia rungu au
panga au bunduki? Je, hiyo si ishara kwamba wewe huna nguvu ndiyo maana
unalazimisha? je, huko si kujikanganya maana umetuambia kuwa wewe ni
Mungu unayeweza yote?)
2.
Je, Allah anapotaka wanadamu wanaomwamini wafanye vita ili kuwalazimisha
wasioamini wamwamini, huko si kutaka msaada kwa viumbe wake?
3.
Sura Al-Shura 42:40
Let evil be rewarded with like evil. But he
that forgives and seeks reconcilement shall be rewarded by Allah.
Aya hii inamaanisha kuwa yule anayemwamini
Allah akitendewa uovu basi anatakiwa alipe uovu, lakini akisamehe atapata
thawabu!
Maswali:
1. Kama aliyetenda uovu anakuwa ametenda jambo baya ambalo halitakiwi na
halikubaliki, iweje lile la mlipa kisasi litakiwe na kukubalika? Huku si
kujikanganya?
2. Lakini
hapo hapo, Allah anasema kuwa mwislamu anayesamehe na kusaka
maelewano atapata thawabu kutoka kwa Allah. Unawezaje kukubali vitu
viwili vinavyopingana? Kwa mfano, unawezaje kusema kuwa, mtu
akikutukana, nawe ukimtukana ni sawa; na
usipomtukana ni sawa!
3. Kikubwa kuliko chenzake ni kipi hapa sasa? Je, ni kulipa kisasi au kusamehe?
Mbona mambo yenyewe hata hayafanani? Yanawezaje kwenda pamoja?
4.
Sura Al-Kafirun 109:1-6
Say, "O unbelievers, I do not worship
what you worship, nor do you worship what I worship. I shall never worship what
you worship, nor will you worship what I worship. You have your own religion
and I have mine."
Yaani,
Enyi msioamini, mimi siabudu mnachoabudu, wala
ninyi hamuabudu ninachoabudu. Mimi kamwe sitaabudu kile mnachokiabudu, wala
ninyi kuabudu kile ninachokiabudu. Ninyi mnayo dini yenu, nami nina yangu.
Pia, quran inasema katika sura Al-Baqara 2:256
There shall be no compulsion in religion.
Yaani:
Hakutakuwapo na kulazimishana katika dini.
LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:
Sura Al-Anfal 8:39
Make war on them until persecution is no more and
Allah’s religion reigns supreme.
Yaani:
Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso
tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.
Maswali:
1. Aliyemwambia Muhammad asiwalazimishe wasioamini kuamini Uislamu ndiye huyo
huyo aliyemwambia afanye vita?
2. Aliyesema kuwa “ninyi msioamini hamtaabudu ninachoabudu” ndiye huyo huyo
anayesema ni vita tu hadi dini ya Allah itawale?
3. Na je, aliyesema kuwa hakuna kulazimishana katika masuala ya dini ndiye
huyo huyo anayesema watu wake wapigane vita?
4.
Huku si kujipinga mwenyewe?
5.
Sura Al-Baqara 2:177
Righteousness is not that you turn your faces
toward the east or the west, but [true] righteousness is [in] one who believes in
Allah ...
Yaani:
Haki (mbele za Mungu) haitokani na mtu
kugeukia mashariki au magharibi. Mtu mwenye haki ni yule anayemwamini Allah ...
LAKINI QURAN HIYO HIYO INASEMA:
Sura Al-Baqara 2:144
Indeed, we see you look repetedly towards
heaven. We will make you turn towards a qiblah that will please you. So turn
your face towards the sacred Mosque (qiblah). Wherever you are, turn your faces
to it.
Yaani:
Tumekuona unavyoelekeza macho yako mbinguni
tena na tena. Tutawafanya muigeukie qiblah itakayowafurahisha. Hivyo, geuzeni
nyuso zenu kuelekea msikiti mtakatifu [japo quran zingine zinasema ‘towards
al-Masjid al-Haram’ – najiuliza 'Haram' maana yake nini!!]
Maswali:
1.
Kama aliyesema aya hizi mbili ni yuleyule; na ni Mungu wa mbinguni,
inakuwaje zinapingana?
2. Kama zimetoka kwa Mungu wa mbinguni, si jambo la ajabu kuona kwamba hapendi
watu waelekeze macho yake kule aliko badala yake waelekeze kwingineko?
3. Kama wewe tunayekuabudu uko juu, kwa nini hautaki tuelekeza macho yetu huko? Huu si mkanganyiko?
4. Na kama wewe ni Mungu uliye mahali KOTE, kwa nini nielekeze macho yangu sehemu moja?
3. Kama wewe tunayekuabudu uko juu, kwa nini hautaki tuelekeza macho yetu huko? Huu si mkanganyiko?
4. Na kama wewe ni Mungu uliye mahali KOTE, kwa nini nielekeze macho yangu sehemu moja?
6.
Sura Al-Nisa 4:135
Believers, conduct yourselves with justice.
Yaani,
Enyi mlioamini, enendeni kwa njia ya haki.
Hapa Allah anazungumzia juu ya haki.
LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:
Sura Al-Nisa 4:129
In no way you can treat your wives in a just
manner even though you may wish to do that...
Yaani:
Haiwezekani kamwe kwa ninyi kuwatendea haki
wake zenu hata kama mngependa kufanya hivyo ...
Maswali:
1.
Aya hizi zinafanana au zinapingana?
2.
Kama hazipingani ni kwa vipi?
7.
Sura Al-Nahl 16:28
The angels will say to those whom they cause
to die in purity, ‘Peace be on you.’ Come into paradise for what you did.
Yaani:
[Kuhusu wale wanaoingia mbinguni] – Malaika
watasema kwa wale ambao watawafanya wafe katika usafi (utakatifu), ‘Amani na
iwe juu yenu. Ingieni paradiso kutokana na matendo yenu.’
LAKINI, QURAN HIYO HIYO INASEMA:
Sura Al-Hijr 15:45-47
Indeed, the righteous will be within gardens
and springs, [Having been told], "Enter it in peace, safe [and
secure]." And We will remove whatever
is in their breasts of resentment, [so they will be] brothers, on thrones
facing each other.
Yaani:
Wenye haki (watakatifu) watakaa kwenye bustani
na chemchemi za maji, kwa amani na usalama wataingia humo. Nasi tutaondoa chuki
yote ndani ya mioyo yao.
Maswali:
1. Katika 16:28, inaonekana kwamba watakaiongia peponi ni watu walio safi kwa
sababu malaika wamesababisha watu hao wafe wakiwa safi. Lakini 15:45-47
inaonyesha kuwa wataingia peponi wakiwa na chuki mioyoni mwao. Je, chuki ni
sehemu ya usafi?
2.
Je, aya hizi zimetoka kwa mtoaji yule yule?
3. Kama chuki ni mbaya kiasi cha kuhitajika kuondolewa mioyoni mwa Waislamu
wanaoingia peponi, iweje wakiwa duniani wanaagizwa kuwachukia wale wasio Waislamu
(kama tulivyoona kwenye 4:101)?
HITIMISHO
Hizi ni baadhi tu ya aya ambazo zinaonyesha
kuwa quran au Allah anasema jambo moja hapa, kisha anajipinga mwenyewe katika
sehemu nyingine.
Na ukweli huu, ninavyodhani,unamaanisha kuwa, ama:
1. Si kila aya iliyo kwenye quran ni maneno ya Mungu muumba vyote – maana
Mungu huyo hawezi kufanya mambo kama hayo; au
2. Quran haitokani na Mungu bali imetokana na chanzo kingine, ndiyo maana
inaonyesha tabia za viumbe za kujisahau au kutojua mambo yote, hususan yajayo.
Nadhani siku ya mwisho Muhammad atawakana watu
wote wanaomwamini maana atakuja kusema kwamba, “Mimi niliwaambia kuwa wakitaka
kujua kama quran inatoka kwa Allah waangalie kama quran inajikanganya. Sasa
waliona kuwa inajikanganaya, lakini wao wakendelea tu kuiamini.
Pia Muhammad atawakana wale wote wanaomwamini
na kumfuata kwa sababu yeye mwenyewe anasema wazi katika sura Al-Ahqaf 46:9,
... nor do I know what will be done with me or
you. I follow only what is revealed to me.
Yaani,
... na wala mimi sifahamu kile
nitakachotendewa wala kile ninyi mtakachotendewa. Mimi nafuata tu kile
ninachofunuliwa.
Swali ni kwamba, je, kama mtu mwenyewe anakiri
kuwa hajui hatima yake wala hatima ya wale wanaomfuata, je, kama ni kweli Mungu
wa mbinguni ndiye aliyempatia quran, je, angekaa kimya kweli juu ya suala la
HATIMA za wanadamu? Yaani jibu la mtu atakuwa wapi MILELE lingeachwa hewani tu
hivihivi? Na kama Muhammad hajui hili na bado anataka watu wamfuate, je, ni
hilohilo tu asilolijua au yapo na mengine asiyoyajua? Bila shaka hii inaashiria
kuwa yako mengi asiyoyajua.
Sijui kwa kweli! Kama nilivyosema, mimi kwa
mambo haya ni maamuma tu. Kwa hiyo, inawezekana niko nje kabisa ya kile kinachomaanishwa.
Nitafurahi kama ndugu zangu Waislamu mtanisaidia kujua mambo haya.
No comments:
Post a Comment