Ukawa,TCD walivyokaribishwa juice na Rais ikulu ndogo mjini Dodoma
Lisu AUMBUKA: Lisu alimtaka Rais kusitisha bunge hilo kwa madai kuwa limepoteza mwelekeo lakini JK alimwambia Lisu kuwa akasome sheria waliyoipitisha kwenye bunge la jamhuri kama inampa rais mamlaka ya kuvunja bunge hilo la katiba.
Jk alienda mbali zaidi akamwambia Lisu, "wewe Lisu ndiye uliyependekeza kuwa Rais mamlaka yake yaishie kuteua wajumbe tu asiwe na mamlaka ya kuingilia bunge kwa namna yoyote ile na nyote kwa pamoja bunge zima la jamhuri mlikubaliana hivyo leo unataka kuniambia nifanye kazi ya kuvunja bunge natumia sheria gani wakati wewe ndiyo uliyependekeza niondolewe hiyo nguvu..."
Kwa mantiki hiyo walikubaliana kuwa wakutane tena tarehe nane ili kila mmoja aangalie sheria gani inamruhusu Rais kuvunja bunge halafu wakikutana kila mmoja aje na hilo jibu.
No comments:
Post a Comment