Mkurugenzi
Mkazi wa ASASI isiyo ya kiserikali ya kupiga vita umaskini Actionaid
Tanzania (AATZ), Yaekob Metena akifungua kongamano la siku tatu kwa
asasi zisizo za kiserikali, wawakilishi kutoka makundi ya vijana na
waandishi wa habari juu ya masuala ya haki kwenye kodi linaloendelea
kwenye hoteli ya Seascape jijini Dar
MAMLAKA mbalimbali ambazo zinawajibika kwa namna moja au nyingine katika kuwezesha mizigo mbalimbali inayoingia nchini kutolewa bandarini zitaunganishwa na mfumo mpya wa kisasa wa kutumia mtandao wa kompyuta wa Tanzania Customer Integrated System (TANCIS) kwa lengo la kuharakisha uondoaji wa mizigo hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja wa elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Diana Masalla wakati akitoa mada katika kongamano
lililoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa bila faida
ikiwa na lengo la kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ)
ikishirikiana na Kikundi cha haki kwenye kodi (Tanzania Tax justice
Group).
Kongamano hilo ambalo linahusu haki kwenye kodi ni sehemu ya mpango wa asasi ya Action Aid Tanzania kuleta uelewa na weledi katika masuala ya kodi miongoni mwa watanzania na walipa kodi ili kufanikisha ukusanyaji wa raslimali zinazowezesha serikali kutoa huduma za msingi na pia kutengeneza fursa za wananchi kujiendesha kiuchumi.
Masalla
alisema mfumo huo mpya ambao utamfanya mwenye mzigo kutoa maelezo ya
mzigo wake kidigitali na maofisa forodha nao kushughulika na mzigo wake
bila kukutana naye ana kwa ana, umeonesha ufanisi mkubwa hasa wa
ufuatiliaji wa hatua kwa hatua tangu mzigo umeingia nchini hadi
unamfikia mhusika. Aidha mfumo huo umebana uchepushaji wa mizigo hiyo
kutokana na ufuatiliaji wa kidigitali unaofanywa na mfumo huo.
Meneja
uratibu na mahusiano wa Action Aid Tanzania Bibi Jovina Nawenzake
akielezea historia fupi ya ActionAid Tanzania na kazi wanazozifanya.
Alisema
ingawa kumekuwepo na kilio kikubwa cha ucheleweshaji wa mizigo na
kusukumiwa lawama hizo TRA, lakini kiukweli kuna mambo ambayo
yanaingiliana na mamlaka zingine na mzigo hauwezi kutolewa mpaka mamlaka
hizo ziseme na kwa mfumo wa zamani ilikuwa inachukua muda kuhangaika
ofisi moja hadi nyingine.
Alisema mathalani kwa bidhaa za pembejeo , dawa na mazao mengine yenye sheria za kimataifa, mizigo yake haiwezi kuingia mpaka TBS au TFDA au wizara husika iidhinishe. Alisema kuundwa kwa mamlaka na taasisi hizo katika mfumo mpya kutasaidia kila kitu kwenda kigitali na hivyo kuharakisha kasi ya uondoaji mizigo bandarini kutokana na kuongezeka kwa kasi ya utoaji wa vibali na ulipaji wa kodi.
Akiwasilisha
mada ya uelewa wa misingi ya kodi na uchambuzi wa misingi ya sera ya
kodi nchini Tanzania, Masalla alisema kwamba mfumo huo pamoja na
kunung’unikiwa Julai mwaka huu baada ya kuzinduliwa Oktoba mwaka jana,
maboresho makubwa yamefanyika ili kuufanya ujibu mahitaji ya wananchi na
walipa kodi.
Miongoni
mwa maboresho hayo ni kuweka kompyuta takribani 20 katika chama cha
mawakala wa utoaji mizigo nchini TAFFA ambapo zinatumiwa na watumishi wa
TRA kuingiza takwimu na kusaidia kujibu hoja za watumishi wa TRA kwa
njia za mfumo wa kompyuta.
Meneja
wa elimu kwa walipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Diana
Masalla, akiwasilisha mada ya uelewa wa misingi ya kodi na uchambuzi wa
misingi ya sera ya kodi nchini wakati wa kongamano hilo.
Masalla
alisema kwamba mfumo mpya unaleta makampuni na mamlaka zote husika
katika mwavuli mmoja na hivyo kurahisisha utoaji huduma na kudhibiti
upotevu wa mapato ya serikali.
Akifungua
kongamano hilo Mkurugenzi mkazi wa Action Aid Yaekob Metena alisema
kwamba ni lengo lao kuhakikisha kwamba kila mtanzania anajua misingi ya
kodi na kwamba bila kodi serikali haiwezi kufanya majukumu yake ya
msingi kama ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya kuzitumia katika kazi
nyingine.
Alisema
kutokana na kukosekana kwa haki katika kodi kumefanya serikali kupoteza
fedha nyingi ambazo zingeliweza kutumika kwa ajili ya kufungua fursa za
ajira na pia kuhudumia shughuli za afya.
Mkurugenzi
huyo alisema lengo kuu la kongamano hilo kutambua misingi ya kodi na
sababu zake na pia kuelewa kwamba kuna haki ya kodi ambayo inamtaka kila
mwananchi na mfanyakazi iwe wa umma au watu binafsi kutambua ushiriki
wake katika kuiwezesha serikali kuwa na makusanyo makubwa ya kodi kwa
maendeleo ya taifa.
Metena
alisema: kama hakuna uelewa wa haki ya kodi na wahusika nao
wakasababisha kodi isikatwe serikali itakuwa inapoteza fedha nyingi.
“Kama hakuna haki katika kodi, serikali haitaweza kukusanya mahitaji yake ambayo yanasubiriwa na watu wake”
Pichani
juu na chini ni baadhi ya washiriki wanaohudhuria kongamano la haki
kwenye kodi lililoandaliwa na shirika la Actionaid Tanzania.
Amesema
mfumo wa kodi unaposhindwa kuwafanya watu wote kushiriki katika
kuitendea haki serikali kwa kulipa kodi ambayo ndiyo msingi wa mapato
yanayochangia maendeleo na ustawi wa jamii.
Kongamano
hilo la Actionaid Tanzania linafanyika katika hoteli ya Seascape
iliyopo jijini Dare s salaam, lengo kuu likiwa kuhamasisha watu kutambua
misingi ya kodi, sababu na serikali yenye makusanyo mazuri ya kodi
inavyoweza kutengeneza fursa nyingi za kiuchumi ili wananchi wake waweze
kuzitumia.
Lengo
la kongamano hilo ikiwa kutanua uelewa na weledi wa washiriki ambao
wengi wao ni kutoka asasi zisizo za kiserikali na waandishi wa habari
wanaotakiwa kujua masuala ya kodi, baada ya mada mbalimbali, ofisa wa
TRA aliulizwa kuhusu misamaha ya kodi.
Katika
kongamano hilo pia waandishi wa walijifunza utendaji wa serikali na
pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha kwamba wadau wenye fedha wanaotoa
michango yao kwa ajili ya bajeti ya taifa na kuboresha huduma za msingi
kwa wakati kwa Tanzania.
Aidha
washiriki wengi katika kongamano hilo walihoji kisa cha serikali
kung’ang’ania Pay as you earn (PAYE) kwa wafanyakazi na kuacha vyanzo
vingine huku misamaha ya kodi ikiendelea kuitafuna.
Wakati huo huo katika mazungumzo na waandishi wa habari Masalla amewataka waandishi wa habari/jamii kufichua wakwepa kodi.
Aidha alisema kwamba sheria mpya ya VAT itaondoa misamaha mingi na hivyo kuisaidia serikali.
Pia amesisitiza wateja wanapofanya manunuzi kudai risiti.
Mkufunzi
wa kongamano la siku tatu la haki kwenye kodi, Bwana Mosses Kulaba
kutoka kituo cha uendeshaji uchumi na sera za biashara, akiwasilisha
mada inayohusu mfumo wa kodi nchini Tanzania na changamoto zake katika
ukusanyaji kodi.
Mmoja
wa washiriki katika semina hiyo aliyeibua hoja ya kuwepo kwa jitihada
za makusudi kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kujikita katika
kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuliko kujikita katika kodi
zilizozoeleka kama PAYE inayolenga kukusanya kodi zaidi kutoka kwa
wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo wadogo.
Ndugu
Anwar Mkama mwakilishi kutoka vyombo vya habari akiuliza swali kwa
meneja elimu kwa walipa kodi juu ya changamoto za mfumo wa kodi nchini
ni namna gani wanazishughulikia ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na
kupunguza urasimu.
No comments:
Post a Comment