Kaimu
Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Mary Meela
akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mikakati wanayoweka ya
kuendelea kudhibiti ubora wa bidhaa nchini ikiwemo kuimarisha ukaguzi kwenye
vituo vya mipakani mwa nchi,Kulia ni Afisa Habari Wa Idara ya Habari Bw. Frank
Mvungi.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akitoa wito
kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuendelea kuelemisha umma kuhusu
madhara ya matumizi ya nguo za mdani za mtumba. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Udhibiti Ubora wa Shirika hilo Bi. Mary Meela
======= ===== =====
Frank
Mvungi-Maelezo
Shirika
la viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuajiri watumishi 200 katika harakati za
kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa shirika hilo Bi Mary Meela
wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Meela amesema watumishi watakaoajiriwa watasaidia kuimarisha utendaji kazi wa
shirika hilo hasa katika kufanya ukaguzi na kuhakisha tatizo la bidhaa hafifu linapungua
au kuondolewa kabisa.
Aidha
Bi. Meela alisema kuwa Shirika limeweza kuweka wakaguzi kwenye vituo 5 ambavyo ni
Sirari, Namanga, Taveta, Horohoro, Bandari za Tanga na Dar es salaam na kuweka
wakaguzi kwenye vituo vya bandari kavu (ICD).
Akizungumzia
kuhusu utumiaji wa nguo za ndani za Mtumba Bi. Meela amewataka watanzania kuwa
mstari wa mbele kupinga matumizi ya nguo hizo kwani zina madhara kiafya kwa
watumiaji na wataendelea kufanya ukaguzi wa nguo hizo na kuziteketeza pindi
zinapopatikana.
Shirika
la viwango lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya mwaka 1975, kasha kuundwa
upya mwaka 2009 sheria ambayo imelipa shirika uwezo mkubwa zaidi wa
utayarishaji viwango na kusimamia utekelezaji wake.


No comments:
Post a Comment