16 October, 2014

ALI KIBA AMPIGA MADONGO DIAMOND KATIKA WIMBO WAKE MPYA

Baada ya kutokuwepo kwa maelewano huku vyombo mbalimbali vya habari nchini vikiripoti bifu/ugomvi unaoendelea kati ya nyota wawili wanaotamba katika mziki wa bongo fleva nchini;Diamond na Ali Kiba. Leo hii  nimekuchambulia kwa undani zaidi nyimbo iliyotolewa hivi karibuni ya Ali Kiba-Mwana ambayo inasemekana alimuimba Diamond.

Hebu ongozana na nami katika uchambuzi wa nyimbo hiyo na kisha acha comment yako chini kabisa.

Tuanze kuuchambua wimbo huo.................................
"Mali ni nyingi nyumbani, kipi kimekukimbiza"
Hapa Alikiba, anamwambia Diamond, nyumbani (SHAROBARO RECORDS) kuna kila kitu, 'beats' kali, Utawala 'Management' nzuri na kila kitu, kitu gani kilimkimbiza SHAROBARO RECORDS?

"Ona babio mamio wote wanakulilia"
 Hapa Ali Kiba anamaanisha kwamba SHAROBARO RECORDS ikiongozwa na Bob Junior pamoja na yeye {Ali Kiba} wote kwa pamoja wanamlalamikia Diamond kwa kitendo chake cha kukimbia kufanya kazi zake katika studio ya SHAROBARO RECORDS  (BOB JUNIOR ALIPIGA KELELE SANA DIAMOND ALIPOKIMBIA SHAROBARO RECORDS )

"Mtoto pekee ako nyumbani, kipi kimekukimbiza" 
Hapa Ali Kiba anamaanisha kwamba Diamond alikuwa ndiye msanii pekee mkali aliyekuwa chini ya Sharobaro Records. Hakukuwa na upinzani wowote ndani ya Sharorobaro Records kitu gani kilimfanya aondoke ? 

"Ona babio mamio wote wanakulilia Ndani ya Dar es salame ulikuja bure"
 Hapa Ali Kiba anamkubusha Diamond kuwa siku alipokwenda Sharobaro Records kwa mara ya kwanza hakutozwa hata senti tano na alirekodiwa wimbo wake buree kabisa. Neno "dar es salame" Ali Kiba amelitumia kumaanisha Sharobaro Records.


Kama ulikuwa haujui, Ali kiba ni moja kati ya Wamiliki wa Sharo baro Records, kwani ana hisa kubwa kati yake yeye na Bob Junior. Na Ali Kiba mdiye alitoa idhini kwa Bob Junior kumruhusu Diamond arekodi bure wimbo wake. Ilikuwa hivi........Diamond alienda kwa Bob Junior na kumwambia ana wimbo wake anaomba urekodiwe lakini hana uwezo wa kifedha. Bob Junior akamuomba kumsikiliza, alipomsikiliza akagundua Dimaond anakipaji, lakini Bob Junior hakuwa na mamlaka ya kuurekodi wimbo huo bure bila idhini ya mkubwa "BOSI" wake {Ali Kiba} ikabidi Bob Junior aende kwanza kuomba idhini kwa Ali Kiba. Ali Kiba akamwambia Bob Junior kama anajua kuimba vizuri amrekodi. Ali Kiba alimwambia Bob Junior hiki "Kama dogo anajua kuimba vizuri, mrekodi tu hakuna shida"

Ali Kiba aliyasema haya kipindi anafanya mahojiano katika kipindi cha mkasi hivi karibuni
Unaweza kuangalia mahojiano hayo ya Ali Kiba katika kipindi cha MKASI TV 
  

"Tena kimwana, kimwana hujui kuchuna"  
 Wakati Diamond anaenda kuomba kurekodi kwa Bob Junior alikuwa tayari kufanya 'show' zake bure ilimradi tu aweze kujitangaza.
Diamond aliwahi kumuomba Ali Kiba apande naye kwenye 'Show' yake bila malipo yoyote ili watu wamuone akiwa na Ali Kiba
Hivyo basi Ali Kiba ametumia maneno  haya katika wimbo wake 
"Kimwana asiyejua kuchuna" masanii mchanga 'Underground' aliyetayari kuimba hata bila malipo.

"Na zile lawama za wale walokuzoeza"
 Hapa Ali Kiba anazungumzia lawama za wasichana mbalimbali wanaotoswa na Diamond.

"Ulikuja jana na leo tofauti sana"
 Hapa Ali Kiba anazungumzia namna ambavyo Diamond alivyobadilika kitabia baada ya kupata mafanikio kimuziki.

"Tena bora Yule wa jana, wa leo tofauti sana"
 Hapa Ali Kiba anawazungumzia Wema Sepetu na Penny, anasema bora hata Penny kuliko Wema Sepetu ambayo yupo na Diamond hivi sasa
  
"Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma"
Ali Kiba anazumgumzia tabia za Wema Sepetu. Mkorofi {dakika mbili mbele nyuma}na Mwingi wa habari ama pasua kichwa {Kichwa kinauma}

"Tena bora Yule wa jana, wa jana leo wa jana" 
 Hapa Ali Kiba anasisitiza anachokimaanisha kwamba kuhusiana na sakata zima la Wema Sepetu.

” tena bora yule wa jana, wa jana leo wa jana ” 
Ali Kiba anamaanisha Wema Sepetu ambaye yuko nae leo na yule aliwahi kuwa nae zamani. 

"Ni wa jana,Upo nae leo,Lakini uliwahi kuwa nae jana"
Huyo ni Wema Sepetu,aliyewahi kuwa na Diamond wakaachana, wamerudiana tena {'Wajana Leo Wa Jana=Wema Sepetu}
  
"Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma"
 Hapa Ali Kiba anakuletea ufafanuzi zaidi kwamba huyu "Wa jana leo wa Jana" si mwingine bali ni Wema Sepetu.
Anaimba hivyo kwa kukuelezea tabia ya Wema Sepetu ambayo ni 'ukorofi''Dakika mbili mbele nyuma'
Kama umesahau ngoja nikukumbushe, Wema Sepetu aliwahi kumtukana Bob Junior matusi ya 'Nguoni',kesi inayoendelea mahakamani hadi hivi sasa. 

"Oyayee Oyayee, mbona unawatesa sana"
Hapa Ali Kiba anamwambia Diamond mbona anawatesa sana hao wasichana anaowabadilisha badilisha 

"Omamee, omame oya mame, omame oya mamee Mbona unajitesa sana"
Hapa Ali Kiba anamuonya kuhusu hao wasichana anaowatesa kwani ni sawa na kujitesa yeye mwenyewe. Kwani inampelekea ashindwe kujua ampende nani katika maisha yale kwa sababu wanawake karibu wote anaotoka nao wanakuwa na kasoro zisizo vumilika. 

"Omamee, oya mame, omame oya mamee Ukaanza kulewa , madawa kuvuta kwa sana."
Hapa Ali Kiba anadhibitisha namna ambavyo hali ya kuwatesa na kuwachanganya wanawake inamrudia Diamond mwenyewe na baada ya kuumizwa na wanawake akaona hakuna njia nyingine ya kupamba na maumivu ya kuumizwa na mwanamke zaidi ya kulewa.
Ikumbukwe kamba Diamond alitoa wimbo uitwao "NATAKA KULEWA" ambao ulikuwa unaelezea kisa cha kweli kilichomkuta Diamond
  
"Ndani ya Dar Es salaam, mambo matamu hayakukwisha hamu"
 Hapa Ali Kiba anaelezea namna ambavyo Diamond hajaishiwa na hamau ya kutembea na wanawake/wasichana ambao anawapata baada ya yeye kuwa maarufu kupitia Muziki.

"We bado mtoto wa mama hujayajua mengi"
 Hapa Ali Kiba anaua ndege wawili kwa jiwe moja;kwanza anatoa ufafanuzi wa mtu anaye mzungumzia .Ali Kiba anataka ujue anamzungumzia Diamond na sio mtu mwingine yoyote yule.

"We bado mtoto wa mama"  
 Hapa Ali Kiba anamaanisha Diamond ni mtoto wa Mama, yupo karibu zaidi na mama yake na hawana mawasiliano mazuri na Baba yake.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...