16 October, 2014

LORI LAPARAMIA WATEMBEA KWA MIGUU BAADA YA KUGONGA MINI BUS



Katika ajali ya kutisha iliyotokea katika eneo la Kaluga, nchini Russia, lori lilikuwa likitembea nyuma ya minibus. Minibus hiyo ilisimama katika mistari ya wavuka kwa miguu, ili kupisha kundi la vijana wanaovuka, waliokuwa tayari katikati ya barabara, wamalizie kuvuka. Nyuma ya minibus, lori hilo, likiwa likitembea nyuma ya minibus kwa ukaribu unaokiuka sheria (tailgating) lilishindwa kusimama na kugonga minibus, kisha magari hayo mawili yakaparamia baadhi ya wavuka kwa miguu, waliokuwa wakijaribu kukimbia kuokoa maisha yao.
Mmoja wa vijana ameumia kichwani (brain damage) na bado amelazwa hospitali. Msichana aliyevaa nguo nyeusi, anayeonekana kugongwa na minivan na kuanguka chini, alitibiwa michubuko aliyoipata na kuruhusiwa kwenda nyumbani siku ya ajali. Bahati nzuri hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...