Wanawake MUNGU atusaidie sana tujue kujenga Mahusiano binafsi ya karibu na MUNGU wenyewe kuliko kutegemea sana kuombewa hovyo hovyo,Kisa tu Umeambiwa na Rafiki yako kwamba yuko Apostle flani ana Upako sana.Ndio ni kweli tuna Matatizo mengi yametusonga yakiwemo Ndoa zetu Watoto wetu,Biashara zetu,na Kadhalika,Na mara nyingi nia yetu ni kufunguliwa kwenye hivyo vifungo vinavyotusumbua. Na shetani yuko karibu sana na sisi kwasababu anajua Nguvu iliyomo ndani yetu, ila wengi wetu hatujielewi.
Ndio maana tunafanyiwa vitu vingi sana kwa jina la kukombolewa na baadhi ya Watumishi kwa imani kwamba tutapona. Na ndio maana kila huduma ya maombezi tuna jaa sisi hivyo inakuwa rahisi sana kwetu kudhulumiwa mambo mengi kwa kujenga imani kubwa sana kwa watu kuliko BABA yetu aliye mbinguni.
Hebu tazama vizuri picha hapo juu, hivi mume wake angemkuta huyo mwanamke akifanyiwa Maombi ya Staili hii "Atamuelewa kweli!?
Tujifunzeni kumlilia MUNGU vyumbani mwetu na tumkumbushe ahadi zake juu ya Maisha yetu na vizazi vyetu.
No comments:
Post a Comment