06 October, 2014

HAUSIGELI AIBA MAMILIONI YA BOSI WAKE NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA


MSICHANA anayefanya kazi za ndani katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, anadaiwa kuiba Sh milioni 2.6 mali ya mwajiri wake.
 
Inadaiwa kuwa siku ya tukio msichana huyo baada ya kuiba fedha hizo, aliruka ukuta wa nyumba na kutokomea kusikojulikana.
Mwajiri wa mfanyakazi huyo, Shujaa Baruti alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 2, mwaka huu saa 3 asubuhi, kwenye Mtaa wa Zaire, Kata ya Endiamtu.
 
Baruti alimtaja mfanyakazi huyo wa ndani kuwa ni Jacquelin Kimario (18) mwenyeji wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, ambaye aliiba fedha hizo na kuruka ukuta wa nyumba na kukimbia na fedha hizo.
 
Alisema msichana huyo alipoiba fedha hizo alitoroka kwa kupanda pikipiki ili akapande gari aina ya Toyota DCM kuelekea jijini Arusha, lakini baadhi ya watu walimkamata na kumkuta akiwa na fedha hizo.
 
“Mimi nimemsamehe na siwezi kumchukulia hatua yoyote huyu msichana baada ya kuniibia fedha zangu ila nafanya utaratibu wa kumrudisha nyumbani kwao Rombo, kwani siwezi kuishi na mtu mwenye tabia hii,” alisema Baruti.
 
Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo balozi wa nyumba 10, Maulid Kimolo alisema ni jambo la kushangaza kwa msichana kuiba Sh milioni 2.6 na wametaka jamii kuwa makini na wafanyakazi wa ndani.
 
Naye msichana huyo Jacquelin alikiri kuiba fedha hizo na kusema alipitiwa na shetani na kwamba alitarajia kuishi vizuri na familia hiyo hivyo anaomba msamaha kwa kufanya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...