21 October, 2014

DALILI ZINAZOASHIRIA MPENZI WAKO BADO ANAMPENDA EX WAKE!

Dalili za hatari ambazo ukiziona kwa mwenzi wako, zinaashiria kwamba bado anampenda ex wake na kuna uwezekano mkubwa bado wanaendelea kuwasiliana. 

1.  Mpenzi wako anamzungumzia ex wake mara kwa mara, iwe kwa mazuri au kwa mabaya.
2. Anazo namba zake za simu. Mapenzi yakishafika mwisho, namba ya simu ya mliyeachana haina umuhimu tena lakini ukiona bado mpenzi wako ameisevu namba ya ex wake kwenye simu yake au ameiandika kwenye diary, hiyo ni dalili mbaya kwamba wanawasiliana. Endelea kuchunguza.
3. Anabadilika ghafla akimuona hata mkiwa pamoja. Yawezekana mpo kwenye matembezi au shughuli za kawaida na mpenzi wako, ghafla ex wake akapita mbele yenu na ghafla mwenzako akabadilika.
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, akakuachia mkono hata kama mlikuwa mmeshikana kimahaba, akatangulia mbele, kubaki nyuma au akamgeukia ex wake, hiyo ni dalili kwamba bado anampenda na kuna uwezekano mkubwa wakawa wanaendelea kuwasiliana.
4. Anajifanya ni rafiki yake wa kawaida. Hakuna urafiki wa kawaida kati ya mtu na ex wake. Ukiona walishaachana lakini bado wanajifanya ni marafiki wa kawaida, lazima ujue kwamba kuna mchezo unaochezeka nyuma ya kisogo chako.5. Anakasirika akisikia ex wake anatoka na mtu mwingine. Hii ni dalili nyingine muhimu, hata kama walishaachana siku nyingi zilizopita, kama bado ana hisia juu ya mpenzi wake wa zamani, atajisikia wivu na kukasirika akisikia anatoka na mtu mwingine. Ataonesha wivu waziwazi, atamchukia, atamsema vibaya na wakati mwingine hata kupigana na mpenzi mpya wa ex wake.
6. Anaendelea kumpa misaada mbalimbali. Ukiona mpenzi wako anaendelea kumsaidia ex wake kama kumtumia muda wa maongezi, fedha za matumizi au kodi ya chumba, ujue bado wanapendana na anafanya hayo kwa sababu anaamini ipo siku watarudiana.
7. Bado anazo zawadi walizokuwa wanapeana kipindi cha nyuma. Ukiona mpenzi wako bado anatunza zawadi walizowahi kupeana na ex wake kipindi cha mapenzi yao, ni dhahiri kwamba bado anampenda.

8. Yawezekana pia kwenye simu yake bado kuna sms au picha walizokuwa wakitumiana kipindi cha nyuma, amezihifadhi hataki kuzifuta! Hiyo ni dalili kwamba bado anampenda.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...