21 October, 2014

UMESIKIA HII KUTOKA KWA BOKO HARAM??

Abuu wa Boko Haram & 200 schoolgirls

Siku chache baada ya vyombo mbali mbali vya habari kuripoti kuhusiana na serikali ya Nigeria na kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram kufanya makubaliano ambayo yalijenga matumaini ya kuachiwa huru kwa wasichana zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kikundi hicho, shirika la utangazaji la uingereza BBC, limeripoti kuhusiana na mashambulizi yaliyofanywa na kikundi hicho.
 
Taarifa zinasema kwamba wapiganaji hao wamewaua kwa kuwapiga risasi na kuwachinja watu kadhaa katika vijiji vitatu tofauti Kaskazini Mashariki ya Nigeria, na kupandisha bendera yao.
Serikali ya Nigeria imesisitiza kuendelea na nia yake ya kufanya majadiliano na kikundi hicho, licha ya kuwa kimekiuka makubaliano waliyoafikiani mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Chad.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...