22 October, 2014

HIVI NDIVYO ALI KIBA ALIVYOMWAGIA SIFA DIAMOND

ali kiba na diamond


Ni siku chache zimepita tangu tamasha la Serengeti Fiesta lifanyike, ambapo tulishuhudia baadhi ya wasanii wa hapa Bongo wakipata nafasi ya kushare stage na wasanii wakubwa wa Afrika kama Davido na Waje huku kutoka Marekani alikua T.I.

Ni ukweli usiofichika kua Fista ya mwaka huu imekua gumzo kubwa hasa baada ya kutokea mzozano kuhusu nani mkali zaidi kati ya Ali Kiba. Japo kulikua hamna ushindani lakini mashabiki wa wasanii hawa wawili wamekua katika malumbano makali.

Ali Kiba alipohojiwa kuhusu wasanii waliofanya poa stejini Alikiba alianza kwa kusema ” Nilichelewa kufika sikuweza kuwaona kina Ommy Dimpoz, Vanessa na kina Young Killer lakini niliobahatika kuwaona wote wamefanya kazi nzuri, nilimkuta Waje na Panto walifanya vizuri japo ni nyimbo zao chache tunazijua ” akazidi kufunguka zaidi kwa kuwataja wasanii ambao anaona yeye walifanya vizuri ” Mr Blue amenifurahisha sana, WEUSI wamefanya kazi nzuri…. kina Diamond wamefanya kazi nzuri pamoja na Linah ”
Hii inaonyesha wazi kuwa Kiba haitaji bifu na mtu ila anaangalia muziki wake ulipo na anapoelekee  kwani mara ya mwisho kufanya mahojiano na mtandao mmoja Ally Kiba alisema anawashangaa watu wanaomfananisha na mtu mwingine huku akiongeza Kiba atabaki kuwa kiba na wao wataendelea kuwa wao.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...