Sehemu ya mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto juzi usiku maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, baada ya kupiga mwereka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani bila ya tahadhari.
Awali, Lori hilo pamoja na kupiga kwake mwereka halikufanya madhara yeyote wala dalili ya kusema litawaka moto. Ila baada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafuta yaliyokuwemo kwenye lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza kabisa lori hilo.
Mbali na hasara kubwa kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na eneo la tukio ambazo zimeteketea kwa moto, Nyumba moja ni ya makazi ya watu, ingine ni duka la jumla la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni. Pia imethibitishwa watu watano wamefariki kutokana na kuungua kwa moto uliosababishwa na mlipuko huo.

Sehemu ya Lori hilo likiwa limeteketea kabisa.

Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.

Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.
No comments:
Post a Comment