06 October, 2014

JOKATE AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE


Jokate Mwegelo ambaye hivi karibuni alishoot video ya wimbo wake wa kwanza kama msanii wa muziki nchini, ametoa sababu za kwanini mpaka sasa video wala wimbo huo havijafanikiwa kutoka.
Jokate a.k.a Kidoti ameuambia mtandao mmoja kuwa video aliyoshoot Kenya imechelewa kwasababu kuna vitu ambavyo hakuvipenda katika video, hivyo vimechukua muda kurekebishwa ili kupata kitu bora zaidi.
“Kuna delay zilitokea kwenye utayarishaji kidogo, sikupenda end product. Cause napenda niwape fans the besssssssst. So nawaomba wanivumilie kidogo. Ndio maana sipo kwenye social networks now, napiga kazi zaidi nisicheleweshe zaidi.”
jokate
Jokate akiwa na Nick Mtuma wa Kenya aliyecheza nae kwenye video yake
Kidoti ni shabiki mkubwa wa Rihanna, pamoja na kuchelewa kutoa wimbo na video yake lakini ameahidi kuwa kabla Riri hajaachia album yake mpya ambayo ni ya nane, yeye atakuwa tayari ameshafanya yake. “Before Rihanna releases her album nitakuwa tayari nishatoa my track…we all love Rihanna”. Alimaliza.
Jokate-video
Jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 lilimpa nafasi Jokate ambaye alipanda na kuimba wimbo wake kwa mara ya kwanza kama msanii wa muziki, wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo jijini Mwanza.
Kabla ya kuamua kuingia rasmi kwenye muziki Kidoti alikuwa tayari amesikika kwenye nyimbo alizoshirikishwa na AY na producer Lucci.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...