Ilianza hivi ndani ya ukumbi wa Bunge...
Anasindikizwa
Muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman baada tu ya kupiga kura ya wazi ya 'hapana' kuhusu Katiba, amekamatwa na watu wa Idara ya Usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar, kama ni kweli anapelekwa Zanzibar.
Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana, ila hali inaweza kuchafuka wakati wowote Visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .
Hali ilikuwa mbaya sana mara baada ya kupiga kura kwani wabunge wa CCM Zanzibar walitaka kumpiga ndio akalazimika kutolewa ukumbini chini ya ulinzi mkali na kufungiwa kwenye ofisi moja akiwa ameandamana na Pandu Ameir Kificho, Balozi Seif Idd, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Baada ya muda aliondolewa hapo akiwa ameandamana na Pandu Kificho kwenye gari yake kupitia lango la Waziri Mkuu akiwa ameambatana na msafara wa maofisa usalama na kupelekwa Uwanja wa ndege.
No comments:
Post a Comment