Mtoto mwenye umri wa siku nane, ameibwa baada ya mama yake kunyweshwa juisi inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.
Mama huyo anayefahamika kwa jina la Bishaliza mkazi wa Dodoma, alijifungua mtoto huyo Jumatano ya wiki iliyopita na kuruhusiwa kurejea nyumbani na mtoto wake siku iliyofuata, wakati anatoka alikutana na dada aliyeomba kumsaidia mizigo michache aliyokuwa na akamkodia bajaji impeleke nyumbani na akaahidi kwenda tena kumtembelea.
Anasema juzi dada huyo alifika nyumbani kwake na akawa amemletea juisi, hivyo alikunywa juisi hiyo na chakula na baadaye akasikia usingizi mzito aliposhituka hakumkuta yule mgeni wala mtoto wake na mlango umefungwa kwa nje
No comments:
Post a Comment