17 October, 2014

KUNDUCHI WAANDAMANA KWENDA POLISI

Picha za waandamanaji wakielekea kituo cha polisi.
KAMERA ya GPL imewashuhudia wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wakiandamana kuelekea vituo vya Polisi vya Wazo na Mtongani, baada ya kudai kuwa ndugu zao wamekamatwa wakiwa hawana makosa na kupelekwa kituoni.
Wakizungumza na chanzo cha habari hii baadhi ya waandamanaji walisema difenda tano za Polisi zilikwenda eneo hilo na kuanza kukamata watu ovyo kwa madai kuwa ni wahuni na wavuta bangi.
Dereva mmoja wa bodaboda alisema kawaida ya Polisi hao hufika na kuwakamata wahuni, wavuta bangi na vijana walio katika makundi ya uhalifu, ila kilichotokea ni wahuni hao kushtuka na kukimbia, ndipo polisi wakaaanza kukamata watu hovyo hata wasiohusika.

GPL

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...