22 October, 2014

MAMBA ALA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI

MWANAFUNZI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Ugalla, Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,  Yohana Ramadhani (14), ameliwa na Mamba wakati akioga na wenzake katika mto Ugalla.


Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Ugalla, Mohamed Asenga, tukio hilo lilitokea Oktoba 18 mwaka huu, saa 11:00 jioni katika mto huo.

Alisema siku  hiyo, marehemu akiwa na  watoto wenzake kama ilivyo kawaida yake, alikwenda kwenye mto huu kwa lengo la kuogelea.

Asenga alisema kuwa, wakati watoto hao wakiendelea kuogelea, alitokea mama mmoja aliyefika mtoni hapo kwa ajili ya kuteka maji, ambapo akiwa anaendelea, alimwona mamba kando ya mto akiwavizia watoto hao pasipo wao kujua.

Kwamba, mama yule aliwaambia waache kuogelea na watoke haraka ndani ya mto kwani amemwona mamba akiwa pembeni akiwavizia.

“Watoto hao walitoka ndani ya mto lakini wakati wakiondoka mamba huyo aliyekuwa pembezoni mwa mto, alimkamata Yohane na kuingia naye mtoni tena,” alisema na kuongeza kwamba zilipiga yowe kuomba msaada ambapo wananchi walijitokeza japo hawakufanikiwa kumuokoa. 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...