21 October, 2014

MBOWE ATOLEA UFAFANUZI PICHA ILIYOSAMBAA MITANDAONI AKIBUSIANA LAIVU LAIVU!!


Wiki iliyopita picha hiyo hapo juu ilienea mitandaoni ikimuonesha Freeman Mbowe na Mkewe Wakibusiana Live ....Mbowe Ameongea haya Kuhusu Picha hiyo :

“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.

Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.

“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,” alisema Mbowe.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...