21 October, 2014

MCHEZAJI AFARIKI AKISHEREHEKEA BAO!


Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kwa timu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jereha la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kupitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na mlinzi mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''Like

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...