Kamati ya Miss Tanzania imesema kuwa haiwezi kumvua taji Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kwa kuwa ni Miss halali na mwenye vigezo vyote vilivyotakiwa, na amewataka watu kutoropoka kwa kuwa hawajui vigezo vinavyotakiwa
Akifafanua kuhusu suala la umri, mratibu wa mashindano hayo Hashim Lundenga amesema kuwa cheti halali walichonacho wao ni kile kinachoonesha Sitti Mtemvu kazaliwa 31 mei 1991 na si vinginevyo.
Kuhusu suala la passport na leseni zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii zikionesha amezaliwa mwaka 1989, Lundenga amesema wao huwa hawangaali vitu hivyo wanachojali ni cheti cha kuzaliwa.
Hashimu Lundenga amesema hakuna suala la yeye kupewa rushwa, ila Sitti Mtemvu ameshinda kihalali kwa kupitishwa na Majaji.
Kuhusu tuhuma za unene amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa...
Habari juu ya sakata la umri halali
wa Mrembo alietwaa taji hilo
Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu.
Lundenga amelitolea ufafanuzi
suala la umri wa mrembo huyo
kulingana na vilelezo alivyopewa
na Sitti Abbas Mtemvu wakati
akijiunga na mashindano hayo
"Katika mashindano yetu,
Washiriki wote hujaza fomu
maalum zilizoandaliwa na Kamati
ya Miss Tanzania. Katika fomu
alizojaza mrembo wa Miss
Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu
amejaza tarehe yake ya kuzaliwa
ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo
kuwa ni sahihi kushiriki
mashindano yetu" Alisema
Lundenga mbele ya wanahabari
hao.
Lundenga aliendelea kusema kuwa
Mashindano ya Miss Tanzania
hayaruhusu mshiriki yeyote
mwenye mtoto kushiri,hivyo katika
suala la Sitti Mtemvu kuwa ana
mtoto,hilo kalina ukweli wowote
bali ni uvumi tu wa kwenye
mitandao ya kijamii baada ya
Mrembo huyo kuonekana akiwa
katika picha na mtoto alieomba
kupiga nae.
Hata hivyo, maswali ya waandishi
wa habari kwa Miss Tanzania
yalizua utata mwingine baada ya
kuonekana cheti kilichooneshwa
kwa waandishi hao
kimetengenezwa September
mwaka huu.
Waandishi walihoji kuhusu cheti
chake cha kuzaliwa cha awali
ambacho alikitumia kupata
passport na leseni ya udereva,
mrembo huyo alisema cheti hicho
kilipotea na alitoa taarifa polisi.
Waandishi hao walipotaka kujua
kituo cha polisi alichoripoti
upotevu wa cheti hicho, alisema
hataki kuzungumzia suala hilo!
Habari juu ya sakata la umri halali
wa Mrembo alietwaa taji hilo
Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu.
Lundenga amelitolea ufafanuzi
suala la umri wa mrembo huyo
kulingana na vilelezo alivyopewa
na Sitti Abbas Mtemvu wakati
akijiunga na mashindano hayo
"Katika mashindano yetu,
Washiriki wote hujaza fomu
maalum zilizoandaliwa na Kamati
ya Miss Tanzania. Katika fomu
alizojaza mrembo wa Miss
Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu
amejaza tarehe yake ya kuzaliwa
ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo
kuwa ni sahihi kushiriki
mashindano yetu" Alisema
Lundenga mbele ya wanahabari
hao.
Lundenga aliendelea kusema kuwa
Mashindano ya Miss Tanzania
hayaruhusu mshiriki yeyote
mwenye mtoto kushiri,hivyo katika
suala la Sitti Mtemvu kuwa ana
mtoto,hilo kalina ukweli wowote
bali ni uvumi tu wa kwenye
mitandao ya kijamii baada ya
Mrembo huyo kuonekana akiwa
katika picha na mtoto alieomba
kupiga nae.
Hata hivyo, maswali ya waandishi
wa habari kwa Miss Tanzania
yalizua utata mwingine baada ya
kuonekana cheti kilichooneshwa
kwa waandishi hao
kimetengenezwa September
mwaka huu.
Waandishi walihoji kuhusu cheti
chake cha kuzaliwa cha awali
ambacho alikitumia kupata
passport na leseni ya udereva,
mrembo huyo alisema cheti hicho
kilipotea na alitoa taarifa polisi.
Waandishi hao walipotaka kujua
kituo cha polisi alichoripoti
upotevu wa cheti hicho, alisema
hataki kuzungumzia suala hilo!
No comments:
Post a Comment