- Mwigulu: "Tutalipa deni la Sh8.4 Tril"
- Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii
Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ya kulipa
madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya
Dawa (MSD).
Mifuko hiyo inaidai Serikali Sh8.43 trilioni. Mfuko wa PSPF
unadai (Sh429 bilioni), PPF (Sh192 bilioni), NSSF (Sh467 bilioni), NHIF
(Sh107 bilioni), LAPF (Sh170 bilioni) na GEPF (Sh6.8 bilioni).
Jumla hiyo ya deni la Serikali linahusisha deni jingine la
PSPF la Sh7.06 trilioni ambayo ni malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa
Fedha, Mwigulu Nchemba alisema kuwa mifuko hiyo huikopesha Serikali
kupitia wizara mbalimbali, fedha ambazo hutakiwa kulipwa baada ya muda
fulani.
Alisema wizara zisipolipa na hivyo deni kukaa kwa muda mrefu, huingizwa kwenye deni la Taifa.
“Madeni hayo ni makubwa, yanahitaji baraza la mawaziri kujadili utaratibu gani utatumika kulipa,” alisema Mwigulu na kuongeza:
“Kwa mfano deni la PSPF ni kubwa na linahitajika kulipwa,
hivyo tunaweka utaratibu lakini siyo kwamba Serikali hailip... kama
mwaka jana tuliilipa PSPF zaidi ya Sh50 bilioni sema nao wana mahitaji
yao.”
Akizungumzia deni la MSD, Mwigulu alisema: “Hili la MSD
tumetaka mchanganuo wa wizara na kila halmashauri jinsi gani fedha
zilizotolewa kwa ajili ya dawa, zimetumika”.
Alisema mwaka jana Serikali ilitoa Sh47 bilioni kwaajili ya
dawa katika wizara na halmashauri, lakini fedha zilizotumika kununulia
dawa ni Sh7 bilioni tu.
“Nyingine wamefanyia mambo mengine na ndiyo maana tunasema
hatuwezi tukawa tunatoa tu fedha bila kupewa mchanganuo wa fedha hizo
zimefanyiwa
[3:18PM, 28/10/2014] Sanga: Mwigulu: Tutalipa deni la Sh8.4 Tril
Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii.
Dar es Salaam. Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).

zimefanyiwa nini,” alisema Mwigulu.
No comments:
Post a Comment