22 October, 2014

NAWAPANGA TU WANAUME - BABY MADAHA

l
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha ambaye anadaiwa kuishi kinyumba na meneja wake Mkenya, Joe Kariuki wa Kampuni ya Candy n Candy Records, ametoa mpya baada ya kudai kuwa kutokana na kusubiri kwa muda mrefu ili apate mwanaume anayefaa kwa ajili ya kumuoa bila mafanikio, sasa ameamua kuwapanga foleni bila kujali idadi yao.

Akipiga stori na chanzo cha habari hii, Baby Madaha alisema amesubiri sana kuolewa lakini hajamuona mwanaume anayefaa, hivyo ameamua kuwapanga kama mafungu ya nyanya kama wao wanavyowapanga wanawake na ikitokea mmoja  ‘akamzingua’ anaachana naye na kumchukua mwingine.

“Mimi sasa hivi nawapanga tu wanaume maana sioni anayenioa ndiyo maana nimechukua uamuzi huu, wanaume wamezoea kutupanga sisi wanawake sasa mimi ndiyo nimewageuzia kibao nao waone utamu wake na ikitokea huyu amenizingua namuacha nahamia kwa mwingine,”alisema Baby Madaha.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...