21 October, 2014

SHKAMOO ROMBO... HARUSI YAACHA GUMZO!

Maharusi  wameacha gumzo baada ya kukodi helikopta kutoka Kenya kunogesha harusi yao na kuruka angani!
Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri katika mji mdogo wa Tarakea uliopo mpaka wa Tanzania na Kenya. Maharusi hao, Lameck Yesse na Gladmarry Mushi walivuta hisia za wengi kwa kuwa bwana harusi ni dereva wa gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah analolimiki na bibi harusi ni mwanafunzi wa chuo jijini Arusha.
Mashuhuda walisema tukio hilo ni la kwanza na la aina yake katika mji huo. Maharusi hao walifunga ndoa katika Usharika wa Tarakea wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), na ibada iliongozwa na Mchungaji Emmanuel Dediok.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...