Baada ya Rasimu ya Sitta kupitishwa na Bunge maalumu baadhi ya wabunge walilipuka kwa furaha na wengine wakakata mauno hadharani, huku mbunge wa Njombe kaskazini Deo Sanga akicheza "Kitorondo" na baadae akamalizia na "msumari" wa Jahazi Modern Taarab.
Mziki huo ulikua ukirindima kupitia simu yake ya mkononi huku yeye akifanya kweli kwa kuonesha "mjini msingi kiuno"
Watu wengi walihamaki kitendo cha wabunge kufurahia Rasimu hiyo hadi kufikia hatua ya kujitoa akili.
Hii hapa siri ya furaha ya Wabunge hao..
RASIMU YA WARIOBA ILIPENDEKEZA:
1. Mbunge akigombea vipindi vitatu basi, awaachie wengine.
2. Mbunge akivurunda katika utendaji wake, wananchi wana uwezo wa kumuondoa na kuchangua mwingine.
3. Hakuna mbunge kuwa Waziri, Mkuu wa mkoa, m/kiti wa bodi ya shirika etc. (kwanini vyeo vyote mjilundikie nyie?).
4. Elimu ya mbunge iwe angalau stashahada (diploma) na kuendelea.
RASIMU YA SITTA (ILIYOPITISHWA) IMEPENDEKEZA HIVI:
1. Ukomo wa Ubunge usiwe vipindi vitatu.. Hata wazee waliokaa bungeni miaka 50 kama Kingunge, waendelee tu kugombea. Vijana wanaotaka kuwa viongozi labda wakajaribu kwenye SACCOSS sio UBUNGE.
2. Mbunge akivurunda wananchi hawawezi kumfanya kitu chochote hadi miaka mitano iishe na mbunge apewe pensheni yake (Mil.160).
3. Ruksa Mbunge kuwa waziri, Mkuu wa mkoa, DC, Mwenyekiti wa shirika, na vyeo vingine kadri anavyoweza kujilundikia. Nyie mnaosema mbunge asiwe na vyeo viwili au zaidi, mna "wivu wa kike" (according to Pius Msekwa), na hampati uongozi ng'o... Labda mkalime vitunguu Mang'ola.!
4. Elimu ya Mbunge iwe kama ya Deo Sanga (mbunge Njombe Kaskazini), yaani kujua kusoma na kuandika tu inatosha. Rasimu ya Sitta inasema si lazima mbunge awe na degree, diploma, au cheti.
Si lazima mbunge awe na elimu ya sekondari. Si lazima Mbunge awe amemaliza elimu ya msingi. Hata kama alisoma akaishia darasa la 3 lakini anajua kusoma na kuandika RUKSA KUGOMBEA UBUNGE.
Sasa je katika mazingira haya wabunge wataacha kukata mauno na kucheza "kitorondo" kwa Rasimu hii kupita??
No comments:
Post a Comment