TAHARUKI imezuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi nchini Kenya, leo asubuhi baada ya abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki dunia muda mfupi alipowasili uwanjani hapo.Abiria huyo mwanamke alikuwa akitokea Juba, Sudan Kusini lakini kukawepo tetesi kuwa huenda amefariki kwa ugonjwa wa Ebola.Vipimo vya madaktari vimeonesha kuwa mgonjwa huyo hakufa kwa Homa ya Ebola. Katibu wa Afya wa Baraza la Mawaziri nchini Kenya, James Macharia amethibitisha kuwa mgonjwa huyo hakuwa na Homa ya Ebola.Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa waliwaona maofisa wa afya wakielekea katika Kliniki ya Port ambapo mgonjwa huyo alikimbizwa kabla ya mauti kumfika.Viwanja vya ndege ni baadhi ya maeneo yaliyo katika uangalizi kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola ambao mpaka sasa umeua watu zaidi ya 4,000 kwenye ukanda wa magharibi mwa Afrika.Shirika la Ndege la Kenya Airways lilisitisha safari zake katika ukanda wa magharibi mwa Afrika kwa kuogopa maambukizi ya ugonjwa huo.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Baada ya miaka 13 ya kuwapo katika fani ya sanaa ya maigizo, hakuna shaka kwamba, Ste...
-
Ever wonder what would happen if we treated our Bible like we treat our cell phone? What if we carried it around in our purses or pockets?...
