Wanafunzi wawili wa darasa la pili wenye miaka saba na mwingine nane wa Shule ya Msingi Kikunku Kigoma wameadhibiwa na walimu wao kutokana na tabia yao ya kufanya mapenzi katika umri mdogo na kusababisha walimu watatu kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto wa kiume.
Akizungumzia tukio hilo mwalimu mmoja wa shule hiyo Nicholous Ulimwengu alisema wazazi wa watoto hao walilamika wanafunzi hao kila siku kuchelewa kurudi nyumbani na kuamua kufuatilia shuleni hali iliyowafanya walimu kuchunguza na kugundua huwa mara baada ya masomo huenda sehemu ya kujificha na kufanya tendo hilo.
Alisema baada ya kugundua tabia za wanafunzi hao walimu waliamua kuwaadhibu kwa kuwachapa viboko vinne kila mmoja ambapo mzazi wa mtoto wa kiume aliamua kwenda kushtaki polisi baada ya mwanae kulalamika kupata majeraha ndipo polisi wakaamua kuwashikilia walimu hao kutokana na adhabu hiyo wakati uchunguzi ukiendelea.
No comments:
Post a Comment