Kwa maelezo ya RPC wa Arusha wakati anaongea na waandishi wa habari alisema, mtuhumiwa wa ugaidi Yahaya Omary alijaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi na ndipo akapigwa risasi ya mguu na risasi ya kiuno wakati akikimbia, kisha akaongeza kuwa mtuhumiwa huyu ndiye aliyehusika na ulipuaji wa mabomu kwenye kanisa arusha, mkutano wa chadema na sehemu zingine mwisho wa kunukuu.
Ukiangalia vizuri mwili wa gaidi huyu utagundua kuwa hakupigwa risasi ya kiuno kama anavyodai RPC bali alipigwa risasi ya tumbo, pia sniper ama mlengaji wa risasi hakuwa nyuma ya mtuhumiwa kama RPC anavyodai bali alikuwa mbele ya mtuhumiwa, ukishaangalia kwa umakini kisha ukaambatanisha na maelezo ya RPC utagundua kuwa hapa kuna mchezo ulifanyika kuficha kitu fulani kama walivyofanya kwa Ulimboka, Mwangosi, Kibanda na wengine wengi haiwezekani mtu anayetuhumiwa kwa ugaidi akasafirishwa kizembe halafu mbunge wa upinzani Halima Mdee mumsafirishe kwa magari 10 ya police yakiwamo ya maji ya kuwasha, askari wa miamvuri na vifaru kama mnaenda vitani,pia RPC anasema gaidi aliyefariki ndiye aliyekuwa anahusika na mabomu yate yaliyolipuka Arusha na sehemu nyingine wakati huo mahakama haijathibitisha hilo.
Tutaendelea kupiga kelele ya kutaka jeshi la police lifanyiwe [OVERAHAUL] lifumuliwe na kusukwa upya kwa utalam zaidi kuna askari wana uwezo mkubwa na wana elimu za juu sana na weredi lakini hawajapata fursa ya kuliongoza jeshi hilo kutokana na mfumo mbovu na badala yake wameweka uwezo na elimu zao kwenye mabegi na kuwaachia makanjanja wachache wasiokuwa na utalam na elimu kuliongoza jeshi hilo
POLICE WALIKUHUKUMU KWA KUKUUWA KABLA YA MAHAKAMA INNALI LAH WAINAILAH RAJIUN
No comments:
Post a Comment