Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) laanza kuuza viwanja takribani 444 vyenye jumla ya mita za mraba 465,161 katika eneo la Kiluvya A Halmashauri ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Hayo yamesema na Meneja Miradi wa NSSF Bw.Abdallah Mseli wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembelea eneo la mradi huo kuona maendeleo ya mradi huo .
“Eneo hili litakuwa na makazi mapya ya kisasa, litakuwa na huduma muhimu za maji,umeme,barabara na pia kuna maeneo ya kujenga shule, zahanati na maduka ya kisasa ” alisema Mseli
Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo Mseli amesema fomu za maombi ya kununua viwanja zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu 40,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kisarawe na Ofisi za NSSF Benjamin Mkapa Pension Towers.
Akizungumzia bei za viwanja Mseli alisema kwa kiwanja cha makazi pekee (ujazo wa juu na kati) gharama kwa kila mita ya mraba ni elfu 15,000/- wakati wakati kwa makazi pekee (ujazo wa chini) Mita moja ya mraba ni 16,000/.
Kwa upande wa Viwanja kwa ajili ya Makazi na biashara Mseli alibainisha kuwa gharama ya kila mita ya mraba ni elfu 17,000/ na vile vya nyumba za ibada vitauzwa elfu 10,000 kwa kila mita ya mraba.
Kwa wale watakaohitaji viwanja kwa ajili ya makazi maalum (housing estate) Mseli alibainisha kuwa vitauzwa shilingi elfu 20,000 kwa kila mita ya mraba.
Naye Meneja uhusiano wa NSSF Bi Eunice Chiume alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo ambayo imetolewa na shirika hilo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kusaidia jamii na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Mradi wa NSSF (Serviced plots) uliopo kata ya Kiluvya-A Madukani Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani una eneo lenye ukubwa wa Hekta 90.5 sawa na ekari 223.6 na una jumla ya viwanja 444 vyenye mita za mraba 465,161.
No comments:
Post a Comment