Polisi nchini Tanzania wanasema watu 7 wameuawa kwa kuchomwa katika eneo la Kigoma magharibi kwa tuhuma za uchawi.
Nyumba za marehemu hao pia zinaripotiwa pia kuchomwa.
Polisi anayesimamia eneo hilo amesema zaidi ya wanavijiji 20 wanaotuhumiwa kushiriki katika kitendo hicho cha kuwashambulia marehemu hao wametiwa mbaroni.
Shirika moja la kutetea haki za binadamu lasema zaidi ya watu 500 hasa wazee huuawa nchini kila mwaka kwa kudhaniwa kuwa wachawi.
No comments:
Post a Comment