Waziri
wa nchi ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma,Celina Kombani,
akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania mjini
Singida. Kombani aliwaasa wahitimu hao 4,960, kwamba wasiridhike na
elimu waliyopata, bali waongeze bidii zaidi katika kujiendeleza.
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZIRI
wa nchi ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma, Celina
Kombani,amesisitiza kwamba serikali haitaajiri wahitimu wo wote kutoka
kwenye vyuo ambavyo havijasajiliwa kisheria.
Amedai
kwamba vyuo ambavyo havijasajiliwa kisheria, vyuo hivyo vinazalisha
wahitimu ‘makanjanja’, ambao serikali haina nafasi nao kabisa.
Waziri
Kombani,aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kilele cha mahafali ya
20 ya chuo cha utumishi wa umma Tanzania yaliyofanyika hapa tawi la
Singida.
Alisema serikali itaendelea kupokea wahitimu kutoka vyo vilivyosajiliwa kisheria, na hasa chuo cha utumishi wa umma Tanzania.
Kuhusu
wahitimu hao 4,960 kutoka matawi yote Tanzania, Kombani aliwaasa kwamba
bado wana safari ndefu katika kujiendeleza kielimu,hivyo waongeze
juhudi kujiendeleza zaidi.
Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi,
akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania
yaliyofanyika mjini Singida. Jumla ya wahitimu 4,960 walitunukiwa vyeti
vya fani mbalimbali.
“Hata
mtakapokuwa mmeajiriwa, endeleni kujielimisha kadri uwezo wenu
utakavyowaruhusu.Ushindani katika ajira ni mkubwa mno,kwa sasa ajira
inahitaji mhusika awe na upeo mkubwa kielimu”,alifafanua.
Awali
mtendaji mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania, Saidi Nassor,
alisema wana mpango wa kupanua chuo kwa kuanzisha tawi jipya mkoani
Mbeya.
“Tutaongeza
madarasa,maktaba za kisasa na ofisi ya tawi la Tabora. Aidha
tunatarajia kuanza maandalizi ya michoro ya kituo kikuu cha chuo
Ikwiriri wilaya ya Rufiji na tawi la Singida baada ya zoezi la fidia
kukamilika kwa aslimia mia moja”alisema Nassor.
Baadhi ya wahitimu wa chuo cha uhazili Tanzania waliotunukiwa vyeti mbalimbali na waziri Kombani.
Kwa upande wa kanda ya ziwa,
Nassor alisema maandalizi ya kupata eneo la kufungua tawi jipya,
yanaendelea vizuri na likipatikana,shughuli za ujenzi zitafanyika.
Wakati huo huo,mtendaji huyo alisema wanaendelea kutoa mafunzo ya ndani kwa watumishi waliomo kazini,kwa lengo la kuwakumbusha kuwa na uelewa juu ya kanuni za utumishi na sheria za matumizi ya fedha za umma.
Wakati huo huo,mtendaji huyo alisema wanaendelea kutoa mafunzo ya ndani kwa watumishi waliomo kazini,kwa lengo la kuwakumbusha kuwa na uelewa juu ya kanuni za utumishi na sheria za matumizi ya fedha za umma.
Baaadhi wa wazazi/walezi na wahitimu wa chuo cha uhazili Tanzania wakijipatia picha kwa ajili ya kukumbukumbu
No comments:
Post a Comment