18 November, 2014

MBUTTAAA!!!...DENTI AKUTWA NA HIRIZI DARASANI!



MTOTO  mmoja wa miaka 9 (jina linahifadhiwa)  ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Manda iliyopo Kijiji cha Mtimbira, wilayani Ulanga, Morogoro wiki iliyopita usiku wa manane anadaiwa kukutwa darasani akiwa na hirizi kubwa kiunoni.

Tukio hilo lilitokea katika moja ya majengo ya Shule ya Msingi Mazoezi Kigurunyembe ya mjini humo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililoshuhudiwa pia na mwandishi wa habari hii, lilijiri Alhamisi iliyopita ambapo mara baada ya kuonekana darasani humo, baadhi ya wananchi walianza kumpa kichapo wakidai kuwa yeye ni mwanga.

Dogo huyo alinusurika kifo kutoka kwa wananchi hao wa Kigurunyembe waliokuwa na hasira kali baada ya mmoja wa walimu kuwatuliza na kufanikiwa kumuokoa mwanafunzi huyo na kwenda kumficha kwenye ofisi ya walimu ya shule hiyo.
Akihojiwa na mwandishi wa habari hii, mwalimu huyo aliyejitambulishwa kwa jina  la Zuhura Khatibu alikuwa na haya ya kusema:
“ Wiki hii mimi ni mwalimu wa zamu nilipofika shuleni nikawashuhudiwa wananchi wakimshushia kichapo mtoto huyo,  kama mzazi niliumia sana nikawauliza kwa nini wanampiga wakadai eti ni mwanga ameanguka hapa shule usiku, sisi tulipigwa butwaa. Nilimuokoa na kumficha ofisini,” alisema Zuhura.
Akizungumza na mwandishi, mwanafunzi huyo alidai kuwa alitokea Mtimbira kwa ndege ya kichawi, anatumiwa na wanga na kwamba alipofika pale shuleni wenzake walimdondosha akaamua kuingia darasani.
Alipoulizwa alikuwa anaelekea wapi usiku huo, alidai walikuwa wakienda Kihonda kwa baba yake anayefanya biashara ya mbogamboga. Alipopekuliwa alikutwa na hirizi kubwa yenye rangi nyekundu kwenye mkanda wa suruali yake, alipoulizwa ilikuwa ya nini alisema alifungwa ili kumlinda.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...