- Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba Mtoto Huyu aliyepigwa na msichana wa kazi anaendelea vizuri
- Tizama Video ya Mateso hapo chini
![]() |
| Baba mwenye mtoto, Erick Kamanzi, (Kushoto), akiwa na watoto wake, Kulia ni mtoto wa miaka 2 aliyepigwa na kuteswa na msichana wa kazi huko Uganda |
MWNAMKE mfanyakazi wa ndani Jolly Tumuhiirwe,
ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alivuma kwenye mitandao ya kijamii kutokana
na kitendo chake cha kinyama cha kumpiga mtoto wa “Mdosi” wake jijini Kampala
Uganda,
amekamatwa na polisi tayari imemfungulia mashtaka ya utesaji.
Hata hivyo polisi wanatoa pendekezo jipya kwa
mwendesha mashtaka nchini Uganda,
ili mashtaka hayo yabadilishwe na kuwa ya kujaribu kuua.
Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 22, alifanya
kituko kisichotarajiwa na wengi walioiona video iliyomnasa kutoka kamera ya
siri iliyotegeshwa na bosi wake bila yeye kujua.
Msichana huyo mzaliwa wa wilaya ya Rukungiri
alikuwa ameajiriwa na Erick Kamanzi ambaye anafanya kazi kwenye shirika moja
lisilo la kiserikali jijini Kampala.
Video hiyo ilionyesha, msichana huyo wa “kazi”,
akimlisha kwa shuruti mototo huyo wa kike mwenye umri wa miaka 2, na kutokana
na kasi ya ulishaji, mtoto huyo alishindwa kuhimili vijiko na hapo akaanza
kutapika.
Kitendo cha mtoto huyo kutapika, kilichokoza
mikono ya msichana huyo, aliyeanza kumzaba vibao vya usoni kabla ya kumrusha
sakafuni na kuanza kumtandika kwenye makalio na kitu ambacho hakijulikani kabla
ya kuanza kumpiga mateke na kumkanyaga mgongoni.

No comments:
Post a Comment