Mwandishi
Jeny Edward anayeripoti kituo cha TVI hapa Arusha amegeuka mwiba kwa
viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini wakiwemo mawaziri,kwa kuwakwida
wampatie fedha wanapokuwa kwenye ziara mbalimbali za kikazi huku
akitumia kivuli cha kuwafanyia interview.
Mfano halisi ni juzi
waziri mkuu,Mizengo Pinda alipokuwa kwenye kongamano la nyuki jijini
Arusha,bila aibu akiwa na mwenzake alimfuata hadi chumbani alikofikia
katika hotel moja maarufu hapa mjini na kumlazimisha ampatie fedha huku
akimweleza kuwa yeye hakulipwa kwenye mkutano huo.
Kana kwamba
haitoshi waziri Nyalandu naye alipata joto hilo hilo kwa kufuatwa kwenye
sehemu ya kupumzikia katika jengo la mikutano AICC akitakiwa ampatie
fedha ,Nyalandu pamoja na kujitetea kuwa hawezi kutoa hela hadharani
,alilazimika kuongozana na mwandishi huyo hadi kwenye gari lake na
kumpatia mshiko wake.
Mimi kama afisa habari wa wizara
nilisikitishwa sana na tabia hiyo hasa baada ya kuelezwa kuwa ndiyo
tabia yake iliyojengeka ya kuwaomba fedha mawaziri,najua hii tabia ipo
sana hapa Arusha lakini nimeambiwa huyu ndo kinara wao ,naomba chama cha
wanandishi wa habari Arusha APC walishughulikie suala la maadili jambo
hilo sio jema,mbaya zaidi alimwagia matusi ya nguoni mbele yangu
mwakilishi wa habari na maelezo wa mkoani Arusha, Prisca Libaga baada ya
kumfuata na kumhoji tabia ya kuwazonga viongozi hadi kwenye magari
akitaka wampatie fedha.

No comments:
Post a Comment