03 November, 2014

UNAFAHAMU NINI KUHUSU NYOTA YAKO???




  • HIVI NDIVYOJINSI WACHAWI WANAVYOWEZA KUIBA NYOTA YAKO


Kuna watu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini?! Wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa Mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! Hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. Unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. Ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani, soma Mathayo 2:1-5. Biblia inasema “Yesu alipozaliwa zamani za mfalme Herode mamajusi wa mashariki walikwenda kumwona, na walipofika wakauliza yuko wapi aliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyota yake nasi tumekuja kumsujudia. Ukisikia mamajusi ujue si watu wema. Kasome biblia ya kiingereza imesema ‘Astrologers’ yaani wabashiri au wanaanga. Pia biblia ya NIV imesema Maggi, yaani washirikina, biblia nyinge imesema the Meggicians yaani wachawi. Kwa tafsri hizi moja kwamoja tunatambua kwamba hawa mamajusi kuwa ni wachawi. Sasa rejea katika kauli yao walipofika kwa Yesu walisema “Yuko wapi waliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyota yake nasi tumekuja kumsujudia” Nifungue akili yako msomaji wa JoJoTheFighter?? Watu hawa ni wachawi, lakini cha ajabu wanasema wameiona nyota ya Yesu wakajua ya kuwa aliyezaliwa ni mfalme. Kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe wachawi wanauwezo wa kutazama katika ulimwengu wa roho na kutambua kwamba wewe una nyota gani katika maisha yako.

Si kwamba walikosea kwa Yesu kusema kwamba Yesu ni mfalme, walisema kweli kabisa rejea kauli za Bwana wetu alipokuwa kwa pilato aliulizwa wewe ndiye mfalme wa wayahudi hakukataa bali alijibu wewe wasema.pia akaongeza kusema kwamba ufalme wangu si dunia hii. kwa hiyo ni mfalme. pia ukirejea katika Isaya 9:6 biblia inasema na uweza wakifalme utakuwa mabegani mwake; Hivyo basi wachawi wakishatazama katika ulimwengu wa roho na kuona nyota yako kuwa ni ya kifalme kama ya Yesu au labda nyota yako ni Biashara, au Elimu, au Ajira,nk. wanachokifanya ni kwamba wanaiba ile nyota na kuiweka kwa mtu mwingine au wakaiacha tu.

Kuna dalili za kutambua nyota yako ni ipi hasa ni rahisi sana kutambua nyota ya mtoto mdogo. kwa mfano: mtoto akiwa na nyota ya uongozi,utambua hivi watafute wanapokuwa wanacheza watoto wengi kwa pamoja, kisha angalia vizuri kaa utulie usipige kelele kisha uangalie vizuri ni lazima atakuwepo mtoto atakayewadhibiti wenzake na kuwalazimisha kufanya anavyotaka yeye na lazima watafanya, kwamfano anawezakusema nyamazeni na wote kweli wakanyamaza, au twendeni na wote kweli wakamfuata.

Pia dalili za kutambua Nyota iliyoibiwa ni hizi, kwa mfano mtoto alikuwa anafanya vizuri kabisa darasani lakini sasa hivi anazidi kudidimia wala hapendi kusoma, ukiona hivyo ujue tayari wameshachukua wanjanja! pia kwa mtu mzima unaweza kukuta kwamba unaandaa mipango lakini haitimii mipango yako. Unapanga mwaka huu lazima nitafungua Duka lakini utashangaa linazuka tatizo hutafungua hilo duka mpaka mwaka utaisha. Au unaandaa mpango mzuri kabisa lakini utashangaa unamwona mwenzako tayari ameshaanzisha mpango uleule kama ulivyokuwa unapanga. au kama ni biashara utaona mwingine kaanzisha vilevile kama ulivyokuwa unafikilia hapo ujue Nyota yako inatumiwa na mwingine. Unajua nyota hizi huambatana na mawazo yako. Jinsi mawazo yako yalivyo ndivyo na nyota yako ilivyo hawezi mtu akaitumia nyota yako pasipo mawazo yako. Utajikuta kwamba wakati mwingine unapoteza fahamu kama hujielewi vizuri vile. Hapo ujue kuna kitu.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...