Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikata
utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa
watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na
Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa
wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya
Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia)
ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda
hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).
Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa HREDP, Abubakar Rakesh akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kushoto), akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri Makamba.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikagua kioski baada ya kukabidhi.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwatunza
pesa wanamuziki ya walemavu ya Bendi ya Tunawajali, iliyokuwa
ikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akijadiliana jambo na baadhi ya wanachama wa HREDP.
Katika
kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel leo imekabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu
wenye ulemavu yenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara
wajasiriamali
Sambambal
na hilo Airtel pia imewapatia mtaji wa kuanzisha biashara ili
kuwawezesha watakao nufaika na vibanda hivyo kuwa mawakala wa huduma ya
Airtel money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel
kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es
Saalam.
Akiongea
wakati wa hafla ya makabidhiano , Naibu Waziri wa mawasiliano Mh.
Januari Makamba alisema” tunapenda kuwashukuru Airtel kwa kutanua wigo
na kutoa msaada kwa watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kujikwamua
kiuchumi. Serikali yetu iko makini katika kuhakikisha kila mtanzania
anapata haki sawa bila kubagua makundi natoa fulsa sawa katika maeneo
mbalimbali.
Sisi
kama Serikali tunaamini msaada mliopokea leo utakuwa chachu ya kuleta
maendeleo ya kiuchumi na nyenzo kwa wanachama wa Taasisi ya haki za
binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu kujikwamu na
tatizo la kiuchumi unaowakumba makundi mengi kama haya katika jamii”.
Sera
ya serikali kwa walemavu inalenga kuboreshea mazingira watu wenye
ulemavu na kuwahusisha katika shughuli za uzalishaji ili kuinua uchumi
na kutumia kwa ufanisi rasilimali zilizopo katika kuboresha huduma.
Naaamini kwa Airtel kuwekeza kwenye jamii leo hakutachangia kuboresha
maisha ya wengi tu bali kutachangia kutekeleza na kutilia mkazo agenda
za Serikali.
Nachukua
fulsa hii kuwaomba makampuni mengine na wadau mbalimbali kushirikiana
na serikali katika kutoa misaada ya muda mrefu na endelevu katika
makundi mengine kama haya nchini kama ilivyofanywa na Airtel leo”.
Aliongeza Makamba
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bibi Beatrice Singano
alisema “ kwa mara nyingine tena tumefikia jamii kupitia mpango wetu wa
huduma kwa jamii tukiamini kwa kufanya hivi tunachangia na kusaidi
familia za wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya
kiuchumi kwa watu wenye ulemavu , pamoja na kuinua uchumi kwa watu wenye
ulemavu kwa ujumla. Airtel tunatoa fulsa na kuwawezesha wale waliokuwa
na ndoto za kumiliki biashara zao kuweza kuzifikia ndoto hizo na
kujikita kwenye ujasiriamali na biashara.
Tunaamini
Msaada huu haujalenga kuwapatia mtaji tu bali vifaa vya kuendesha
biashara pamoja na mafunzo ya jinsi ya kuendesha biashara endelevu.
Tunauhakika ushirikiano tulioanzisha leo utawaweza wanachama wa kikundi
hiki kuwa sehemu ya kutoa huduma zetu na hivyo kupata faida
itakayowawezesha kuwa wajasiriamali bora nchini’.
Tunawaasa
wale wote watakaofaidika na msaada huu leo kutumia vibanda hivi kwa
ubunifu na kuhakikisha vinawanufaisha kufikia malengo yao ,bado
tutaendelea kushirikiana pamoja nanyi na jamii kwa ujumla katika
kuhakikisha tunatimiza lengo letu la kuboresha maisha ya watanzania
kupitia huduma na bidhaa zetu za kibunifu na fursa za kibiashara’
aliongeza Singano.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya
kiuchumi kwa watu wenye ulemavu Bw. Abubakar Rakesh alisema”
tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa kupata rasilimali
muhimu za kuanzisha biashara.
Tunawashukuru
Airtel kwa msaada huo na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuwa cha kwanza
kupata msaada kama huu . Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia
nafasi hii vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na
kufanikiwa katika biashara zao”.
“Napenda
kutoa shukrani zangu za pekee kwa serikali na kwa Mh Makamba,kwa
mchango wake na kujitolewa kwake kuwasaidia watu wenye ulemavu”
aliongeza Rakesh
No comments:
Post a Comment