Mrembo Zari anayedaiwa kuchukua nafasi ya Wema Sepetu akiwa ameshika tuzo za Diamond.
Diamond Platnumz akipozi baada ya kutwaa tuzo tatu za Channel O jana usiku nchini Afrika Kusini.
Diamond Platnumz akiongea machache baada ya ushindi huo wa kishindo.
Diamond katika pozi na wadau.
Diamond katika pozi na wadau pamoja na mama yake mzazi, Sandra (wa pili kulia).
Diamond (katikati) akiwa na management yake. Kulia ni Said Fella na Babu Tale (kushoto).
Mama mzaa chema, Sanura 'Sandra' Kassim katika pozi.
Kutoka kushoto ni Mama mzazi wa Diamond 'Sandra', Diamond na Zari katika picha ya pamoja.
MSANII
Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametwaa tuzo tatu za Channel O jana
usiku nchini Afrika Kusini. Tuzo hizo ni; Most Gifted new comer, Most
Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One.
Kupitia ukirasa wake wa Facebook Diamond amewashuru sana mashabiki wa wote walio msupport.
"Kiu
kweli, haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na
support kubwa mliyonipa iliwezesha Bongo Flavour yetu kuandika historia
mpya kwenye ramani ya muziki wa Afrika...Hii inaonyesha ni jinsi gani
umoja ni nguvu na pia jinsi gani muziki wetu ukisupportiwa na kupewa
kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi... Shukrani sana kwa
@channeloafrica @channelotv kwa kuniona na kuthamini kipaji changu, My
Family, Management, Media zote zilizokuwa zikinisupport, Watangazaji,
Wasanii, Wadau na bila kuwasahau wapendwa wangu" - Ameandika Diamond.
Askari wa JKT akutwa
mferejini akiwa kalewa chakari .....Pombe Ilipozidi alianza kujisaidia
ndani ya basi
12/01/2014 12:01:00 AM Shaban R Dege 0 KITAIFA
Katika hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT)
anayesadikika kuwa ni wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa usiku wa jana amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada
ya kukutwa amelewa chakari na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo
la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa
Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema
kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa
amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.
Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha
kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha
katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga
huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe
kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja
ndogo ndani ya basi hilo.
Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua
hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji
kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji
machafu .
Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu
yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa
nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumtukana akilishushia
heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza
"Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare,
sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho
kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina
wala cheo chake hakukitaja.
Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na
kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana maombi ambayo
aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la
Kihesa.
Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Make Money at : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment